Msaada Malipo ya Sasa ya DSTV

Msaada Malipo ya Sasa ya DSTV

Kuna ADTv wa Abdhabi unaangalia soka,movies n.k. full HD dollar 100 kwa mwaka,ila gharama kubwa ni mwazo yaani installation Decoder,dish ect ni kama $700.

Duh. hii ndo kwanza naisikia leo! tupe detail wanapatikana wapi hao?
 
Lipia compact plus ni nzuri sana unapata 90% ya footbal kama wewe ni mpzenzi wa mpira.

Kiasi gani hiyo? nasikia unapata SS10, ambaye ni pacha anayefanana sana na SS3
 
Wadau naombeni msaada.

Nahitaji kufahamu malipo ya Premium na Compact packages kwa sasa ni hela ngapi.

Nimewapigia Customer Care bila mafanikio.

Halo wakubwa,naombeni mnijulishe bei ya decoder fully installed ya dstv kwa sasa.shukrani
 
Kuna ADTv wa Abdhabi unaangalia soka,movies n.k. full HD dollar 100 kwa mwaka,ila gharama kubwa ni mwazo yaani installation Decoder,dish ect ni kama $700.

Kaka hii imekaa vizuri, hawa watu wanapatikana wapi, unaweza kuorodhesha channels walizonazo? Pia kama utaweka contucts itakuwa powa zaidi!@
 
Nina namba zao zote.

Tatizo ni kuwa wana ku-hold on muda mrefu...Mhudumu hapokei simu na hela inakatwa!
Hiyo ndo customer care ya kampuni za kibongo bana,wanakuweka kwenye simu mpaka hela yooooote inaisha
 
hawa jamaa ni washenzi, siku za nyuma walikuwa na pakeji mbili za mpira premium (ile yenye SS3 ambayo ndo inaonyesha mechi nyingi kubwa) na compact. mara ya mwisho nakumbuka ilikuwa unalipa 120000 kwa premium na compact kwa 45000, hiyo compact ilikuwa unaweza kuona mechi kibao tu. saiv wameivunja premium na compact na kuzalisha compact plus ambayo kwa sasa wanachaji 77000.kwa sasa simshauli mpenda mpira kununua hiyo compact haina lolote.
 
Jamani jamaa kaomba mmpe payments now, mbona mnaziunguka. Compact plus ni $ 48 ambayo kwa mwezi huu nimelipa 78000/= na premium wanalipia $ 78 ambayo kwa sasa ni kama 126000/=
hizi $ hazibadiliki ila Tsh ndo inachange daily.
 
Back
Top Bottom