Msaada Malipo ya Sasa ya DSTV

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Wadau naombeni msaada.

Nahitaji kufahamu malipo ya Premium na Compact packages kwa sasa ni hela ngapi.

Nimewapigia Customer Care bila mafanikio.
 
premium ina range kwenye 125,000-130,000, compact 45,000. inategemea na kupanda kwa dollar
 
Lipia compact plus ni nzuri sana unapata 90% ya footbal kama wewe ni mpzenzi wa mpira.
 
Lipia compact plus ni nzuri sana unapata 90% ya footbal kama wewe ni mpzenzi wa mpira.

Bila ya hii kitu nisingehangaika na hawa watu. Ni wasumbuf sana hasa km umepata tatizo na unahitaji msaada wao. Mpira, ubora na uwingi wa chaneli zao ndio unaonitia pingu na hawa jamaa vinginevyo ningeachana nao kuna dekoda kibao mtaani saivi.
 
premium ina range kwenye 125,000-130,000, compact 45,000. inategemea na kupanda kwa dollar

Haya malipo kwa kutegeme na exchange rate ya dollar tanzania yataisha lini? Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa hili swala lilishajadiriwa bungeni na waziri mkulo akasema hairuhusiwi na inatakiwa kuachwa mara moja!! Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nani mwenye jukumu la kufuatilia utekelezaji wake? Mbona I.M.T.U watoto wa maskini wanalipizwa tuition fees kwa dollar? Mnisaidie wana JF.
 
Sheria zipo wazi kabisa kuhusu hii kitu. Usimamizi ndo umekuwa tatizo. Juzi kati nilikuwa kwa Madiba hawaruhusu matumizi ya pesa nyingine zaidi ya hela yao Rand. Ukija na hela zako, ingia byuro kwanza ndo ufanye matumizi FULLSTOP!
 
Jamani mbona hawa jamaa wana gharama kiasi hicho? Hivi haiwezekani kuchakachua hizi decorder za hawa jamaa kama wanavyofanya kwenye umeme?
 
Jamani mbona hawa jamaa wana gharama kiasi hicho? Hivi haiwezekani kuchakachua hizi decorder za hawa jamaa kama wanavyofanya kwenye umeme?

sidhani!

Makaburu wako smart sana kwenye menejimenti ya faranga. the moment unalipia tu ujue hiyo ela ishasomeka kwenye system zao bondeni! Vivyo hivyo kwenye luku.

Ni ngumu sana kuwatoboa.
 
Jamani mbona hawa jamaa wana gharama kiasi hicho? Hivi haiwezekani kuchakachua hizi decorder za hawa jamaa kama wanavyofanya kwenye umeme?

Tatizo kubwa la watz hatuna ushirikiano. Kila mtu anaumia kivyake.

Nakumbuka Uganda mwaka jana wateja wa DSTV waliandamana kupinga matumizi ya dola na kupanda kwa bei mara kwa mara.
 
Kuhusu matumzi ya dola anayeumia zaidi ni Serikali yenyewe kwa sababu ndo mnunuzi mkubwa kuliko wote.

Japo mwisho wa siku tunarudi palepale hizo pesa wanazipata kwa kodi tunazokatwa wananchi.
 
hawa jamaa wametukamata pabaya wamejihakikshia soko na wanajua watu hawana kwa kukimbilia. kama ni mpenz wa mpira ni lazma utachagua unanunua pakeji zao vinginevyo kacheki mechi baa. kifupi wanaringa na hawana jitihada za kuboresha huduma zao

customer servis yao ni hovyo
wanatoza kwa dola
bei zao ndo hizooooo
 
Kuna ADTv wa Abdhabi unaangalia soka,movies n.k. full HD dollar 100 kwa mwaka,ila gharama kubwa ni mwazo yaani installation Decoder,dish ect ni kama $700.
 
Back
Top Bottom