Kwa Maoni yangu
1. Usiwe unaishi maeneo ya Uswahilini... haya ni maeneo ambayo ni hatari sana wakati mtoto anakuwa.. Kama ni mtoto wa kike Na hili nimeliona Sana na kulishangaa nilipokuwa naenda kutembelea watu.. unakuta mtoto wa kike anakkushika Zipo ya Suruali n.k inabidi umchape na kumkanya kwa hasira
2. Jaribu kuishi mahali ambapo hakuna msongamano wa Watu wengi na Patulivu.. mahali patulivu ni sehemu nzuri sana ya kulelea watoto
3. Weka Limit katika TV ya Nyumbani na Ukiona Kuna Vipindi vibaya vya kimaadili Jaribu kuvicontrol au Weka Password kabisa kama watumia DSTV... yaani kwa kifupi weka Parent Control
4. Kama Watoto wanasoma Hakikisha wanazingatia masomo kwa Wewe mwenyewe kuwa karibu nao na kuwafundisha.. mfano unaweza kumwambia alete daftari lake na unaangalia alipokosa then Unakaa naye na Kuanza kumfundisha..
5. Angalia ni kina nani hasa anacheza nao... mfano unaweza kukuta anacheza na watoto amabo ni watukutu na wakorofi.. tafadhali vunja uhusiano huo.. maana unaleta madhara kwa Watoto wako.. wanaweza kuiga Matendo yao..
6. Mtoto akifikia miaka Miwili Usilale naye yaani wewe na mkeo msilale naye kitanda kimoja.. tafuteni utaratibu alale na wenzake.. maana watoto huanza kujifunza mambo mengi wakifikia umri huo...
7. Kuna wazazi huwa wanaona sifa sana kuwapeleka watoto wao Sehemu za starehe na mkusanyiko wa watu ili wapate raha... mfano kumbi za starehe, swimming n.k.
Mi naona sidhani kama unamjenga mtoto kiakili bali unamfunza Maovu maana anaona Watu wakiwa Nusu Uchi na Wakati wewe huwa unamfundisha ajisitiri na aone Aibu akiwa Uchi ila Unakuwa wa kwanza Kumpeleka Maeneo ambayo Watu wapo nusu uchi kabisa...
8. Usimbane sana mtoto maana hili linaleta madhara baadae.. siku nyingine muache afanye Mwenyewe na anapokuwa anaelekea pabaya mkanye na umwambie Kuwa si vizuri kufanya jambo fulani.. mfano sometimes anaweza akawa ana Graduate shuleni kwao na Siku hiyo kuna Disco baadae Usimkataze kwenda kwenye Disco la Gratuation yao bali mwambie Awahi kurudi Nyumbani asichelewe...
Ila Mtoto anapoanza Kuwa na Tabia ya Kuenda disco mara kwa mara Na unaanza kuona Si kawaida mkataze na mkane asiwe anaenda kabisa.......
HIVYO NDIVYO NILIVYOLELEWA HATA MIMI...