Msaada: Lotion nzuri kwa uso wenye mafuta

Queen Horse

JF-Expert Member
Sep 12, 2013
414
317
Habari zenu wana urembo,

Naomba msaada wa kupewa ushauri wa moisturizer gani nzuri kuupaka usoni kwa wale wenye combination skin or oily skin uso wangu una mafuta ambayo hayachemki bali yanaganda na kutoa weupeweupe flani hivi usoni.

Sio siri unaninyima raha rangi ya ngozi yangu ni brown naomba katika ushauri huo mnisaidie mositurizer ambayo itanifanya ngozi yangu ibaki hivyo hivyo brown coz sipendi kujichubua kabisa.
 
Nina uso wa mafuta lakini sio ya kuganda . Napaka Nivea ile kubwa kopo jeupe. Trust me hutojuta
Haibadili rangi kabisa ni nzuri sana . Bei 28-30 thousands.

Pia nakushauri ukitoka mizungukoni ukirudi home baada ya kuoga usipake mafuta.
 
Inapatkana wapi hiyo nivea maana nasikiaga kunakuwaga na fekero
 
Nina uso wa mafuta lakini sio ya kuganda . Napaka Nivea ile kubwa kopo jeupe. Trust me hutojuta
Haibadili rangi kabisa ni nzuri sana . Bei 28-30 thousands.

Pia nakushauri ukitoka mizungukoni ukirudi home baada ya kuoga usipake mafuta.
inaiwaje hasa hiyo nivea,tofauti yake na nivea zingine kwa muonekano ni zipi?
 
Queen, ni muhimu pia kutumia both cleanser and scrub kabla ya ku moisturize, inasaidia sana kupunguza mafuta.
 
Habari zenu wana urembo,

Naomba msaada wa kupewa ushauri wa moisturizer gani nzuri kuupaka usoni kwa wale wenye combination skin or oily skin uso wangu una mafuta ambayo hayachemki bali yanaganda na kutoa weupeweupe flani hivi usoni.

Sio siri unaninyima raha rangi ya ngozi yangu ni brown naomba katika ushauri huo mnisaidie mositurizer ambayo itanifanya ngozi yangu ibaki hivyo hivyo brown coz sipendi kujichubua kabisa.
Watu wenye mafuta mengi usoni nawashauri waanze kwa kuyapunguza mafuta kwanza kabla ya kuhangaika na vipodozi vingine kama lotion na cream.
Kuna poda zinaitwa POND'S (Oil Control Talc) hizi husaidia sana kupunguza mafuta na kufanya ngozi ya mtu kuwa ya kawaida na inayokubali vipodozi vingi zaidi. Poda hii ni nafuu sana (Sh 3,000/= - 3,500/=) na hupatikana kwa urahisi kwenye maduka mbalimbali ya vipodozi, cha msingi iwe original na iwe OIL CONTROL TALC.
Sambamba na poda hizo kuna sabuni za PEARLS ambazo ni mahususi kabisa kwa ajili ya kupunguza mafuta.
Pia nawashauri mtumie FACE WASH/CLEANSER, husaidia kuondoa uchafu unaoziba matundu ya kutokea jasho na mafuta.
Epuka scrub, hususan kama haupaki mafuta. Maana baada ya hapo mwili utazalisha mafuta mengi zaidi.
Kwenye uchaguzi wa lotion nashauri tafuta lotion ambazo zimeshauriwa na kuandikwa FOR OILY SKIN.

Kwa ushauri zaidi na huduma za urembo na vipodozi basi mnaweza mkakaribia kwenye ukurasa wa facebook uitwao S&E BEAUTY SOLUTIONS na kuLIKE ukurasa huo kwa habari na mafunzo zaidi.
Mawasiliano : 0 659 528 724 na 0 784 082 847

Nawatakia kila la kheri katika kujipodoa na kupendeza!
 
Apricot scrub ni nzuri kuoshea uso baadaye paka Nivea cream ni nzuri ninaitumia zaidi ya miaka 18 sasa
 
Jaribu kutumia kunyasi [Astringent] kama hii ambayo ni mahsusi kabisa kwa watu wenye nyuso zenye mafuta.

Ina kiwango cha asilimia 2 ya salicylic acid, kemikali ambayo hutumika kuondoa na kuzuia chunusi, kuondoa mabaka ya usoni, na kutibu matatizo mengine ya ngozi kama vile psoriasis, ichthyoses, na kadhalika.

k2-_8a4ec24b-3002-4f88-9445-d951a412562c.v1.jpg
k2-_24985112-e7f5-4427-aec8-e65a49723269.v1.jpg
 
Back
Top Bottom