Msaada: Kwenye Ajira portal nimejaza bado inasoma 92% completed. Ni nini tatizo?

Upo sahihi sana.
Hayupo sahihi hawajasema uweke original certificate ila wanataka uweke copy ya original certificates ambayo umepeleka kwa mwanasheria ana piga mhuli wake unakuja una scann then una upload.
Hili ni kosa ambalo vijana tunashindwa kuelewa vitu vidogo kama hivi unashindwa zingatia mtu usipoitwa unasema umerogwa au unakuja sema UTUMISHI hawako fair wakati mchawi mwenyewe unabishana na vigezo sasa ukipewa kazi kweli utaweza kuifanya sitoi kejeli ila jaribu kuzingatia ulichoambiwa maana walishawahi kulizungumzia hilo UTUMISHI la vyeti na ku sign.kila la kheri
 
Academic certificate inayowekwa muhuli ni orgina au copy before scanning process??,
Toa copy vyeti vyako mkuu nenda kwa wakili apige muhuri uje scann kisha upload hiko origina hakiguswi na utaenda nacho siku ya usaili tu kuhakiki basi mbona jambo linaeleweka vijana wenzangu maana hata mtoto wa darasa la kwanza ukimpa haya maelekezo atayapokea vizuri kuliko vijana waliofika na kutunukiwa shahada ni kweli hizi shahada za miaka hii zina shida gani UTUMISHI mbona wanajitahidi kutuhimiza kufata taratibu zao ila bado hatutaki kuelewa anyway kila la kheri fata maelezo na kuwa serious
 
Heri?

Napata tabu kidogo sijui ndio iko hivyo au la , kwenye ajira portal ujazaji wangu wa taarifa binafsi na makorokoro kibao bado ina soma 92% completed.

Kuna uwezekano huenda sija wahi kuitwa kwenye usahili wa ajira za serikali kisa hii 92%? Au ni mpaka ifike 100%?

Au kuna kitu sija kiweka sawa walau basi isogee hata 95% kama sio 98% hata 100% kabisa.



mimi ninachokifahamu ukifikisha kuanzia asilimia 70 unaitwa kwenye saili zao kama una sifa za nafasi ya kazi husika. ila pia kama kuna changamoto inakukatiza unaweza kuwapigia simu zao za mikononi wamekuwa wakizitangaza mara kadhaa, au kuwatembelea pale maktaba kuu ya taifa gorofa ya pili wako poa wanakuelekeza hatua kwa hatua ukifika uliza kitengo cha TEHAMA au Mawasiliano Serikalini utapata msaada.
 
JINSI YA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA AJIRAPORTAL NA KUJAZA TAARIFA MUHIMU
kwa maelezo zaidi pitia link ifuatayo inaelezea hatua kwa hatua kuanzia kujisajiri (registration) na kujaza taarifa zako inahusisha picha ambazo zitakuwezesha kujua wapi unashindwa au unakwama wapi pia jinsi hiyo profile itakavyoweza kufika angalau 70 uweze kuitwa kwenye usaili
link:Jobtipstz: JINSI YA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA AJIRAPORTAL NA KUJAZA TAARIFA MUHIMU
So ukishaa declare, huwezi kufanya changes zozote. ? Maana mm nimejaribu lkn kile kijitiki hakitoki Na wala haiongezeki imebaki 54% tu
 
Nimejaza nafasi (vipengele) vyote lkn imegomea 54% only! Tatizo liko wapi? Msaada plz kwa anayejua vizuri plz
 
MSAADA!Nimetengeneza Account kwenye Ajira Portal!Nimejaza Vyote ambavyo ni Hakika Ila Inasoma 54% wananikatalia Kuapply Mpka Ifike 70%. by the way nimemaliza Chuo Last Year Au Ndio Tatizo
Kuna sehemu hujajaza mkuu lazima ufikie 79 kama huna experience yeyote,weka attachments zako mfano Cv,na Birth certificate pia vyeti vyako usisahau kila unapojaza education level,passport yako pia ebu tulia alafu anza kujaza tena lazima ufike hizo 79% na zaidi japo unaweza usifike 100%
 
mimi sioni wapi natakiwa kuattach cheti cha fom6 na 4
msaada tafadhari maana nikienda kwenye other attachments kuna CV, Birth certificate na Barua tu
 
Back
Top Bottom