Habari zenu waungwana, kwa wataalam na wazoefu au ambaye amewahi kupatwa tatizo kama lililonikuta tafadhali naomba msaada wa kitaalam na kiufundi pia, ninatumia simu ya Tecno Phanto 6 Plus toka mwaka jana, kuna siku walinitumia OS Latest Vision nikai -download ila nilipo maliza kui-install simu yangu ilianza tatizo nikimpigia mtu simu hanisikii na wakati mwingine ninasikika kwa sauti ya chini sana na kulazimika kuongea kwa sauti kubwa ili angalau niweze kusikika. Naomba msaada ili niweze kutatua tatizo hili.