mbwangali
JF-Expert Member
- Jan 8, 2021
- 1,828
- 3,276
Habari za wakati huu wanajukwaa. Nimepatwa na tatizo la kupata maumivu kwenye joints za mikono ( zilizokaribu na viganja vya mkono).Tatizo lilianza mwanzoni mwa mwaka huu ila maumivu nilikuwa nayapata nikishika kitu kwa nguvu au nikivunja kitu kwa nguvu kwa kutumia mikono.
Nilikwenda hospital nikapaewa dawa aina mbili (Febuxostat na Meloxicam)ambazo nilitumia mwezi mzima na nilipata nafuu kidogo tu lakini tatizo liliendelea.
Nilirudi tena hospital nikapewa dawa nyingine inaitwa Calcivita pamoja na Meloxicam. Nimemaliza kuzitumia week iliyopita lakini bado napata maumivu.
Nina mpango wa kwenda hospital nyingine tena ila nimeona kabla ya kwenda ni vema pia nikiomba msaada na ushauri kwa wenye ujuzi hapa jukwaani kwasababu kuna member aliwahi kuomba msaada wa dawa ya kutibu tatizo fulani ambalo na mimi nilikuwa nalo hivyo nilifuatilia kwa makini wadau waliotoa ushauri na tiba hapahapa jukwaani na mimi nikafuata ushauri ule na nikapona kabisa lile tatizo langu, hivyo naamini hata kwa tatizo hili la sasa naweza kupata msaada.