Msaada: Kwa waliowahi kufunga ndoa ya Serikali

Anayefungisha: Msajili wa Ndoa
Masharti:
1. Asiwe ndugu yako,
2. Asiwe mke wa mtu,
3. Isiwe ndoa ya mkataba, au ya muda mfupi
4. Asiwe mtoto. Kama unamke lazima ajulishwe na atasign kwenye mkataba wenu wa ndoa
5. Ndoa itatangazwa kwa siku 21
6. Ni lazima uwe na wasimamizi wakati wa ndoa
Wengine waongeze..
 
Ok katika hizo form mtahitaji muende na barua za utambulisho zenye picha zenu toka serikali za mtaa..yaani wewe na mkeo/mmeo tarajari.
Siyo mtaa..wanataka barua kutoka ofisi ya Kata.
 
Nenda Na mwenzi wako Ofisi ya Mkuu wa wilaya ambayo mnategemea kufunga ndoa yenu mkifika pale mtapewa maelekezo yote Na msajiri wa ndoa.
 
Ndoa zote ni za serekari mchungaji au shehe wanapewa dhamana ya kuiwakilisha serekari kwenye Ndoa hizo mkuu
 
Kumbe hizi nazo matangazo mpaka siku 21 kama kanisani? Mi nikajua unalipia 50000 then unafunga ndoa!
 
Hii ya serikali ntafunga kumbe ni simple tu
Tena mkiamua mnabeba mtu yeyote yule mtaani kwenu na sio lazima iwe public, unaambiwa ukitaka ndoa ya haraka unalipia 100,000/= tu ndoa inafungishwa baada ya kulipa.
 
Kumbe hizi nazo matangazo mpaka siku 21 kama kanisani? Mi nikajua unalipia 50000 then unafunga ndoa!
Mchungaji au shehe anafungisha ndoa kwa niaba ya serikali, na anae toa cheti cha ndoa ni serikali yenyewe.

Tunaenda kanisani/msikitini kwa sababu za imani zetu tulizo nazo. Maana ukifunga ndoa ya serikali kwenye dini hiyo ndoa haitambuliki.
 
Ndoa zote ni za serikali, na ndio maana cheti kimeandikwa Jamhuri.........na nembo ya Taifa Tanzania......sema ni nyie mnataka kufunga kwa namna gani , Bomani, Masjid au Kanisani........taratibu zote zinafanana.........kumbuka iwe kanisani au masjid......tangazo lazima litoke kwenye ubao wa matangazo wilayani (Bomani)
 
Mkuu Mtui kwenye process ya kufunga hii ndoa ya bomani, kuna kuvishana pete?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…