Kama umefunga system yako ki-standard, yaani Kutoka kwenye panel kwenda kwenye charge controller, halafu charge controller to battery na charge controller kwenda kwa matumizi ya taa, itakuwa rahisi kujua shida iko wapi.Mchana taa ya kuonyesha panel inafanya kazi (kawaida ni green na iko kushoto) itakuwa inawaka kuonyesha kuwa panel inaleta umeme kawaida. Taa ya kati huonyesha nguvu ya betri. Kama betri iko sawa, itakuwa njano kidogo na ikijaa itakuwa blue, na taa ya tatu ni ya umeme kwenda kwennye matumizi, Hii ikizimika ujue hakuna umeme unaoenda.
Kwa maelezo yako inaonekana betri imekufa, Ukitaka kuhakikisha hilo, jua likwaka hata muda mfupi uaona betri imejaa, lakini jua likipotea tu betri inakuwa down. Ungekuwa mtaalam ningekueleza kuwa betri ikijaa, disconnect panel halafu washa taa utaona zinazimika haraka.
Betri za kujaza maji huwa zikienda chini ya volt 10.6 mara kwa mara, huwa zinakufa hata ukijaza maji upya ni bure. Nakushauri ununue betri isiyotiwa maji (VRLA NON SPILABLE - DEEP CYCLE). Kwa panel uliyonayo ya 50W na matumizi yalivyo, betri yako isizidi 80AH
Usipoelewa niulize, na hata ukishanunua hiyo betri usiifunge kama wewe si mtaalamu, waweza kuunguza charge controller au hata nyumba yako