mdida
JF-Expert Member
- Jul 14, 2011
- 1,607
- 775
WanaJF kama somo linavyosema hapo juu, ninapokuwa mjamzito huwa Napata maumivu makali ya mgongo/kiuno japo sio mara kwa mara. Naweza kuumwa mara moja kwa wiki au mara mbili. Na hayo maumivu ndio hunishtua kuwa ni mjamzito. Ila safari hii yamezidi. Nilikuwa na mimba ya miezi mitatu bahati mbaya nikawa naumwa hicho kiuno/mgongo hadi juzi nikashtukia damu inaanza kutoka kufika hospital mimba ikawa imetoka. Hayo maumivu ya safari hii ilikuwa ni kila siku au baada ya siku mbili naumwa. Yaani ule mgongo wa kushtua ndani ya dakika mbili hadi unatokwa jasho. Je wadau nisaidieni nini tatizo au nifanyeje kuondokana nalo?