Msaada kwa huyu binti, anaumia

Msaada kwa huyu binti, anaumia

anaekutaka humtak haumpi nafac,
[HASHTAG]#fidQ[/HASHTAG]
mapenzi ndivyo halivyo sjui kwa nn
 
Hivi kidato cha tatu tulikuwa tunaruhusiwa kufanya mapenzi? Dah kumbe mama yangu alikuwa mkali zaidi ya Simba. Siku hizi kawa mpole wadogo zangu hawakuonja hili joto.

Maana nakumbuka alinambia nikipewa barua nimpe. Na nisipompa atajua na atanivunja miguu . kwahiyo sikupokeaga barua yeyote. Dah sio kwa mikwala ile.
 
Naona jamaa anamfananisha huyo Bint na tabia ya Ndugai
 
Watu na mioyo yao.
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Mwambie ajiunge JF tumshauri vyema.

Mimi nina maswali ya nyongeza ningependa kumuuliza.
asisahau kuni-tag akija tafadhali.
Fursaaaaa. [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Binti jamani amefika hadi chuo ila ameshindwa kuelewa kitu kidogo kama hicho. Msaidie kumwambia jamaa amesha sahau vitu vya sekondari [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hii sio ishu kubwa ya kitafuta ushauri jadi jf....ni simple tu hakuna mapenz tena hapo
 
Atambue kakua sasa na yuko chuo na si o-level,.hata uwezo wake wakufikiria ni muhimu na lazima ubadilike! Aache mapenzi ya ahadi, asome kwa bidii atapata mwanaume mzuri hata humu watamfata.
 
Huyo rafikiyo ana tabia za kupe hapendwi ila kang'ang'ania tu
 
Mwambie dada asilazimishe king, atakuja jutia baadae. Huyo kijana wa kiume hana time nae na vema akakubali matokeo na kusonga mbele.
 
Amna kitu kigumu kwenye mapenzi kama kukubaliana na ukweli, hali halisi, hichi ndo kinacho mkumba uyu dada kwa sasaivi, cha msingi inabidi akubaliane na hali halisi tu, apo hakuna mpnz tena
 
Ahadi za kidato cha nne na binti wa kidato cha 3 ni kwamba walikua wanaota ndoto bila usingizi.hawajui mapenzi wala maisha walikua wanasumbuliwa na utoto.
Jamaa kakua anajitambua mwaka wa3 chuo kashampata anaeota nae ndoto za kiutu uzima.halafu na wewe jiongeze mzigo wako huo eti unamuombea ushauri badala ya kujiweka au msukuma wewe??
 
Nina rafiki yangu wa kike ambaye tumeshibana sana kiasi ambacho ananishirikisha hadi mambo yake ya kimahusiano. Hivi karibuni amenieleza yanayomsibu/anayopitia kwa sasa.

Ameanza kwa kunieleza kwamba wakati anasoma O-Level (Boarding) alikutana na mwanafunzi wa kiume aliyekuwa anasoma shule ya jirani na aliyokuwa akisoma yeye. Ingawa huyo wa kiume alikua amemtangulia kidato kimoja. Walipendana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi. Walipendana kiasi cha kupeana ahadi nyingi za kuja kuwa na familia hapo baadae. Na kwa wakati wote walipokuwa kwenye mahusiano wakiwa shuleni, walikutana kimwili mara moja.

Siku zilisogea na hatimaye yule kijana wa kiume akamaliza kidato cha 4 na kurudi kwao Moshi(Mchaga), akamuacha huyu binti anamalizia mwaka wa mwisho, naye akamaliza na kurudi kwao Dodoma(Mgogo). Baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano kati yao. Maana hakuna aliyekuwa na simu.

Huyu binti akafanikiwa kwenda Advance akamaliza na kufanikiwa kwenda chuo. Alipofika chuo bila kutarajia akakutana na yule mpenzi wake akiwa mwaka wa pili. Kilichomshangaza huyu binti ni ile hali ya yule kijana, hakuonyesha kumchangamkia/kufurahi kwa kukutana tena baada ya kupotezana kwa muda wote wa zaidi ya miaka miwili akizingatia kwamba walipendana na kupeana ahadi nyingi tamu. Kwa wakati wote huo binti aliamini ipo siku watakutana na kuendeleza uhusiano wao maana alimpenda yule kijana kwa dhati.

Ni mwaka mmoja sasa tangu wakutane hapo chuoni, maana binti ameingia mwaka wa pili na kijana ndio amalizia mwaka wa tatu, lakini kijana hana muda kabisa na huyu binti kwa mwaka mzima, zaidi ya salamu tu. Amejaribu kumwambia waonane ili waongee lakini kijana haonyeshi kujali kabisa. Amemkumbusha kuhusu uhusiano wao lakini jamaa hana habari. Yaani hana time kabisa na huyu binti.

Kinachomuumiza kumuona kila siku mtu ambaye anampenda sana lakini yeye hajali kabisa. Amekuwa akijaribu kumvuta karibu kimawasiliano kwa kumpigia simu na kumtumia text mara kwa mara lakini imeshindikana. Na kwa sasa ameamua atulie tu maana ni kama amekata tamaa, lakini anaumia sana, anajiuliza maswali bila majibu kwamba ni nini hasa kimempata huyu kijana, kikapelekea akabadilika kiasi hiki. Japo anasema bado ana matumaini kidogo kuwa inaweza kutokea wakarudi kama zamani.

Je, upo uwezekano wa huu uhusiano kurudi tena kama mwanzo????

Kwa kuangalia mtiririko mzima wa hii story, je, yule kijana alimpenda huyu dada kwa dhati???

Na Je, afanye nini???

Hebu wadau jaribuni kutoa maoni yenu kwenye hili, nami nitamfikishia. Hii ni story ni ya kweli kabisa na dada yupo kwenye wakati mgumu sana.

Naomba wakuu mtoe maoni yaliyojaa hekima.

KARIBUNI.
Ni PM
 
Back
Top Bottom