Msaada kwa hili

hamuka

Member
Jul 18, 2012
5
0
Ndugu wanajamii forum , naomba kuuliza kama chuo kimefungwa , kutokana na matatizo, ni taratibu gani zinafuata baada
ya hapo?

Chuo cha maendeleo ya jamii Mlale kilichopo Songea kilifungwa mnamo tarehe 4/6/2012 na mpaka sasa tamko halijatolewa kwamba chuo kitafunguliwa lini. Baadhi ya matatizo yaliyopelekea kufungwa kwa chuo hicho ni kama yafuatayo.
- Kutokuwepo kwa huduma safi ya maji , huduma ya umeme licha yakwamba unatumika kwa somo la ICT , kutokuwepo kwa huduma ya afya .

Hayo ni baadhi tu ya matatizo yaliyopelekea kufungwa kwa chuo . Lakini kubwa zaidi Mkuu wa wilaya hiyo Ndugu Josephu J. Mkirikiti siku alipotoa tamko la kufunga chuo alisema, sababu kuu ni kwamba chuo cha maendeleo ya jamii Mlale hakina hadhi ya kuitwa chuo.
 
Back
Top Bottom