Msaada kwa anayeweza kumdhamini huyu mwanafunzi tafadhali

KB THE DON

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
243
108
Habari za kuamka wakuu lakin pia nitumie nafasi hii kuwatakia heri ya Sikukuu ya SABA SABA bila kuwachosha na maelezo mengi.

ifuatayo ni sms ambayo nimetumiwa na kijana wa kitanzania ambaye niliwahi kumsaidia jambo kidogo nilipokutana naye kwa bahati tuu katika mapambano yake kielimu

''Baba apo sijui wanishaurije yani me apa sielewi kwasababu nilikuwa najisomesha mwenyewe nilipoamua kurudia mtihani nikawa nafanya vibarua kupata ada na nauli, wanyumbani wameshakataa kunisomesha wanasema uwezo tena hakuna apa nashindwa elewa kwa O level nlfaulu vzuri nilipata DIV TWO YA point 19 ila2 baada yakwenda advance hali ikanpata nkaxhndwa fanya mthan wangu vzur wa mwixho Kipind kile nasoma alikuwa ananisaaidia mdogo wangu wa kike aliyekuwa anafanya kazi za majumban dar ila kashaacha kaolewa
ikawa ndo kama chanzo cha mimi kuhangaika mpaka sasa hapa inaniwea ngumu tena nashindwa elewa nianze wapi tena make mimi.

Hasa tatizo ada nyumbani uwezo wa kumudu kulipa ada hamna mana baba nguvu hana tena tulikuwa twategemea kilimo ''.

Sasa maelezo ya ziada ni kwamba kijana huyu alipofaulu kidato cha nne kwa kupata div 2 ya 19 alipokwenda advance akisomea PCM (akisaidiwa na dada yake aliyekuwa house girl huko Dar ambaye kwa sasa ameacha kazi yake ameolewa) hakufaulu ndipo alipoamua kujisajili kama mtahiniwa binafsi kwa matokeo yaliyotoka now amepata div 3 ya 15ni kipindi ambacho nimepata kumfaham kutoka na na mahangaiko yake ya kutafta fedha kwa hali na mali kulipia tution na nauli kwenda kusoma hadi alipo fanya mtihani wake.

Sasa anataman kuendelea masomo lakin ndoto zake zimezimika kwa sababu ya hali ngumu ya maisha waliyonayo katika familia, nataman sana kumsaidia lakin uwezo sina hvyo nikaona bora kushare hap a endapo anaweza kupatikana msamalia mwema kumsaidia hata kwa kuandikishana mkataba maana dogo anacomitment sana lakin pia endapo kuna ushauri mnaweza kuutoa hapa jinsi gan anaweza fanikiwa huyu kijana.

Naomba kuwasilisha
 
Kikubwa kama ni mtoto wa kiume apambane....Kwanza mawazo ya kusoma for now aweke pembeni...ajikite kwenye kutafuta namba ya kuishi kisha kusoma kupo tu atakuja kusoma hata miaka ya mbeleni huko ..kuliko now anapigania kusoma kwa shida...akimaliza nako KAZI inakuwa kupata KAZI ..so apambane angalau apate kajikazi au kamradi kake...maisha yatasonga Mungu atamjalia atakuja kusoma mbeleni huko
 
Kikubwa kama ni mtoto wa kiume apambane....Kwanza mawazo ya kusoma for now aweke pembeni...ajikite kwenye kutafuta namba ya kuishi kisha kusoma kupo tu atakuja kusoma hata miaka ya mbeleni huko ..kuliko now anapigania kusoma kwa shida...akimaliza nako KAZI inakuwa kupata KAZI ..so apambane angalau apate kajikazi au kamradi kake...maisha yatasonga Mungu atamjalia atakuja kusoma mbeleni huko
Umemaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom