Msaada kuwezesha kilimo changu

uroto

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
404
250
Habari ndugu wana JF

Mimi ni mkulima,nimelima vitunguu na nilipandikiza tarehe 27 march,hivyo mwezi wa 7 mwanzoni nategemea kukivuna kitunguu changu (maji)

Lengo la kuandika uzi huu ni kuwaomba msaada,kitunguu changu kuna maeneo kikubwa sana hasa eneo ambalo nililima chainizi mwaka jana

ila eneo ambalo sikulima chochote kitunguu kimekuwa ni kidogo tofauti na chenzake

hivyo naomba mnisaidie angalau nipate mbolea ya CAN mfuko mmoja na dawa aina ya CALANTURA lita moja ambayo inauzwa 30,000..

mimi ni mkulima mdogo bado nimelima heka moja na nusu,,hvyo mwenye kunisaidia kiasi cha 130,000 mimi kati ya tar3-10 july ntakua nshakitoa,basi ntamrudishia

mpaka nmkuja hapa basi nimekwama ndugu zanguni,niazimeni hata kwa riba mi niko tayari,maana Mungu akijaalia naweza nikatoa gunia 50+ nakuendelea

Mimi ni kijana mdogo miaka 23 nimesota sana mpaka kuamua kufanya kilimo na nnaamini ndo mkombozi wangu

watu wengi naowafata wanasema hawana hela kutokana na kuniona sina chochote zaidi ya kupigika shamba

mnisaidie kwa riba ili namimi nitakapo kitoa angalau nijitanue zaidi kwenye kilimo

msaada wenu tafadhali,nimejidhiki nikapata mbegu,nkauza kuku zangu nikanunua mbolea,,nikauza simu nikapata madawa na borster,,leo hii sina tena chakuuza na kitunguu kilipofikia kinahitaji mbolea ya mwisho angalau kitanuke

NAPATIKANA HOMBOLO DODOMA..Mungu awatangulie
 
Umkontho

Member
Jun 3, 2017
5
45
Nawaza tuu hii post ya jana mpaka leo hakuna anayejibu...... Kwa mtazamo wangu nawaza mengi hapa, assume mtu yuko Ruvuma, mwingine yuko Kagera. Alafu hapa tuko kwa ID feki maana members wengi humu zaidi ya 98% hawatumii majina yao halali..... Sababu ni nyingi. Tafuta hata saccos au watu wa vicoba. Mimi naamini watu wanaokopesha kwa riba wapo ila hujajua namna ya kuwapata.. Jichanganye broo. Tatizo hapa mtu akikutumia labda awe ameamua tu kucheza karata, kwani hata usiporudisha atakupataje... LABDA APATIKANE ANAYETOA MSAADA TUU, ASIYEWAZA KURUDISHIWA
 
asante kwa ushauri mkuu,,nmeshafanikiwa kupata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom