Naomba kujua ni jinsi gani ya kusajili gari ambalo lilikuwa linatumika nchi nyingine kama Kenya, Burundi n.k,, ili niwe nalitumia Tanzania kwa namba za Tanzania.
Naomba kujua mlolongo mzima na gharama zake. Samahani kwa anaejua ama kwa TRA.
Kwanza unatakiwa uwe na certificate of DE-REGISTRATION, kutoka nchi husika, Yaani kwa mfano gari ulikuwa unaitumia tz sasa unaipeleka Kenya, lazima tra waiondoe kwenye mfumo wa usajili wa tz ili iwe huru, pili unatakiwa uwe na barua ya interpol kutoka nchi husika ambapo gari hilo linatoka ili kuthibitisha kwamba hilo gari c la wizi, na tatu ukishakuwa na hivyo vitu Utampa wakala wa forodha hizo nyaraka pamoja na invoice ili aweze kuzipeleka tra akadiriwe kodi ulipe ndio usajiliwe gari lako tayari kwa kulitumia. Asante...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.