Msaada: Kupotea kwa vyeti vya kidato cha 4 & 6

Msaada: Kupotea kwa vyeti vya kidato cha 4 & 6

Muhode

Member
Joined
May 7, 2013
Posts
12
Reaction score
4
Habari ndugu wanajamii,

Nimepotelewa na vyeti vyangu vya baraza (form 4 na form 6) kama miez miwili au mitatatu hivi.Kwa kipindi chote hicho nimekuwa nikivitafuta bila mafanikio.Kutokana na hilo naomba kujuzwa kwa yoyote yule anayefahamu kuhusu mambo yafuatayo.

1.Kujua utaratibu wa baraza juu ya jambo hilo

2.Kuna mtu ameniambia kwamba baraza huwa wanatoa statement of results na sio cheti tena,je ni kweli?na kama ni kweli vp kuhusu hizi ajira hususani za serikalini wanazodai hawapokei statement of result ndo kusema haturuhusiwi tena kuomba?au wanaelewa?.

Naomba mwenye uzoefu na hili anisaidie tafadhali.NIKO KWENYE HARD TIME SANA NDUGU ZANGU.
 
Habari ndugu wanajamii.
Nimepotelewa na vyeti vyangu vya baraza (form 4 na form 6) kama miez miwili au mitatatu hivi.Kwa kipindi chote hicho nimekuwa nikivitafuta bila mafanikio.Kutokana na hilo naomba kujuzwa kwa yoyote yule anayefahamu kuhusu mambo yafuatayo.
1.Kujua utaratibu wa baraza juu ya jambo hilo
2.Kuna mtu ameniambia kwamba baraza huwa wanatoa statement of results na sio cheti tena,je ni kweli?na kama ni kweli vp kuhusu hizi ajira hususani za serikalini wanazodai hawapokei statement of result ndo kusema haturuhusiwi tena kuomba?au wanaelewa?.Naomba mwenye uzoefu na hili anisaidie tafadhali.NIKO KWENYE HARD TIME SANA NDUGU ZANGU.

Utaratibu uko hivi:

1. Unatoa taarifa polisi, nao wanatoa taarifa kwenye media na baada ya muda maalum (sikumbuki ni siku ngapi) kwa mujibu wa taratibu za kipolisi utapewa statement ya kuthibitisha kupotea kwa vyeti vyako kisha unaipeleka baraza la mitihani.

2. Baraza la mitihani wataipitia statement iliyotoka polisi na kujiridhisha kama ni kweli na ikithibitika kua ni kweli basi utaandaliwa statement ya baraza kila unapohitaji kupeleka vyeti vyako sehemu husika (kama vile kwenye usaili wa ajira).

3. Inapotokea tangazo la kazi na likasema statement hazihitajiki nadhani ni zile zitolewzo kabla ya vyeti kutoka lakini kwa hizi za vyeti kupotea nadhani zinakubalika ingawa sijawahi kufuatilia kujua hilo ila kama utapata nafasi wasiliana na tume ya utumishi wa umma kupata maelezo zaidi kuhusu uhalali wa kutumia au kutotumia statement ktk ajira za serikali.

Kwa hayo machache natumaini utakua umepata pa kuanzia ila hapo kwenye red ni kweli kabisa.
 
vinapatikana, nipm nikupe utaratibu japo sio rasmi sana
 
muhode hapo juu kaeleza vizuri sana...kuhusu tangazo ni kwamba lazima liwe gazeti linalotambulika kiserikali...lisiwe la udaku, then tdangazo likae kwa muda wa mwezi mmoja kwa uchache...na statement of results hupewi wewe...atatumiwa aliyekuomba hivyo vyeti,i.e kama unaaply chuo hivyo mkuu wa chuo ndo atatumiwa...wewe kazi yako ni kumfuatilia huyo mkuu kama keshatumiwa. pole sana ndugu. Pia ni mhanga wa kupotelewa chet cha f4
 
Back
Top Bottom