X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,346
- 14,169
wakuu ni matumaini yangu kuwa mpo salama wasalmini...kutokana na hali ya kiuchumi na kutafuta ajira bila mafanikio, na kutokana na kusubiri ajira za serikali bila mafanikio, nimeamua kuanzisha kilimo cha umwagiliaji drip irrigation....kitu pekee nilichokuwa nacho ni ardhi yenye zaidi ya heka 4. na endapo nitaweza kuliendeleza hilo shamba naweza kupata zaidi ya heka hizo...ila sina mtaji wa kuniwezesha kupata vifaa {kuchimba kisima, kununua mabomba, pipe na pump}. nahitaji kulima kisasa kabisa hivyo lengo langu ni kulima kwa msimu wote wa mwaka...mazao nitakayoyapa kipaumbele ni nyanya, vitunguu, mihogo naa pilipili...kama kuna mtu mwenye kujua jinsi nitakavyoweza kupata mkopo zaidi ya 10m kwaajiri ya huo mradi tafadhali naomba uniunganishe.