Msaada: Kumpa maziwa ya ng’ombe mtoto wa miaka 2

jadit

JF-Expert Member
Oct 4, 2019
273
212
Habari wana JF wenzangu, samahani naomba mnisaidie naweza kumpa maziwa ya ng'ombe mtoto mdogo wa miezi miwili?

Na kama naweza kumpa naomba mnisaidie nayachanganya vipi ili nimpe natanguliza shukrani
 
Wanashauri ni hadi afike mwaka mmoja.

Swali langu kwa wachangiaji wengine ni kwamba kwanini maziwa ya lactogen ya south africa yanazuiwa sana. Na ni bei poa sana
 
Habari wana jf wenzangu, samahani naomba mnisaidie naweza kumpa maziwa ya ng'ombe mtoto mdogo wa miezi miwili?? Nakama naweza kumpa naomba mnisaidie nayachanganya vipi ili nimpe natanguliza shukrani
Kwa uelewa na uzoefu wangu mtoto wa miezi miwili mfumo wake wa chakula haujakomaa na pia hauwezi himili maziwa ya ngombe. Ndiyo maana kama maziwa ya mama hayapatikani kuna maziwa ya unga ambayo yana virutubisho kwa viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mtoto mchanga.

Jaribu kwenda kituo cha afya au zahati/clinic ya watoto wana uzoefu na cases kama hizo upate uhakika wa asilimia 100.
 
Wanashauri ni hadi afike mwaka mmoja.

Swali langu kwa wachangiaji wengine ni kwamba kwanini maziwa ya lactogen ya south africa yanazuiwa sana. Na ni bei poa sana
Miezi 6 sio mwaka
Ila ikiwa mama anachangamoto ya kiafya
Anaruhusiwa kutumia.

Inapendeza afuate ushauri wa daktari na kuudhuria kliniki kila tarehe tajwa ilo kufatilia AFYA ya mtoto

Lakini kama mama hauna CHANGAMOTO zozote za kiafya usimpe kinachotakiwa ni wewe mama kula VYAKURA vyenye virutubisho vya mlo kamili ili kukuwezesha kutoa Maziwa kwa wingi yenye uzito na ubora mzuri(muhimu pia hata tendo la ndoa msifanye kwa fujo kwa ajiribya afya ya mtoto).

Achana na habari za kusema mtoto ashibi maziwa.

Katika miezi mie4 ya mwanzo mtoto anahitaji sana maziwa ya mama pasipochanganywa na chochote Even MAJI ili kumtengenezea KINGA YA MWILI ukuaji mzuri wa mtoto pamoja na kumantain Kilo za mtoto kuongezeka
7bu miezi 6 ya mwanzo ndipo utakapojenga AFYA ya mtoto ambayo ndo inabeba mistakabari na taswira NZIMA ya maisha yake
 
Turudi ktk Asili yetu.
Kwani mama mtu ana tatizo au majukumu?
Tafuta mama anayenyonyesha jirani hapo mlipe akunyonyeshee mtoto na tafuta kipump Cha maziwa mama anaweza kutumia kuhifadhi maziwa sema huyo mnyonyeshaji azingatiwe TU lishe.
Maziwa ya mama hufanya watoto kuwa na akili timamu na msongo au kutokujiani ukubwani husaidia.
 
Back
Top Bottom