Msaada; Kuku kuchangia kiota kimoja cha kutagia

Msaada; Kuku kuchangia kiota kimoja cha kutagia

Risk takker

Member
Joined
Feb 28, 2015
Posts
19
Reaction score
6
Niwatakie Jumapili njema, Kuna tatizo linanisumbua kutokana na kuku wangu wa kienyeji kutaga sehemu moja kwa pamoja (Kuku wawili hata watatu wanataga kwenye kiota kimoja). Nimejaribu kuweka viota vingi kwa ajili ya kutaga lakini bado wanalundikana kwenye kiota kimoja. Naombeni msaada wakuu mwenye ujuzi na hili swala..
 
Waache watage ingawa ni changamoto kubwa kwani hupiga kelele wakiwa katika foleni ya kutaga.

Cha kufanya kwenye hivyo viota vipya jaribu kuweka yai/mayai kadhaa ili kuvutia hao wengine kutagia.Ikishindikana waache watagie pamoja then utawetenganisha wakati wa kuatamia. Hapo pia pana changamoto kwani wanaweza kuhamia sehem moja. Cha msingi ni kuwa monitor kila mara mpaka watapozoea sehem zao.
 
Asante mkuu ntafanya hivyo.
 
Kumbe tupo wengi, tatizo mmoja akianza kulalia yule mwingine nae anafosi kulalia hata kama muda ulikua bado.
 
Tatizo linalonipata lingine kuku wangu hawan sehemu maalumu ya kutagia, leo atataga hapa kesho pale, kesho kutwa Sehemu nyingine, naombeni msaada nifanyeje ili kila mmoja awe na sehemu yake ya kutagia
 
Kwenye hivyo viota vingine ulivyotengeneza hamishia mayai hata matatu matatu hivi ili kuwavutia kwenda kutaga, akiinga kutaga akakuta mwenzie tayari yupo anataka atataga sehemu nyingine na ataizoea, mimi sio mfugaji sana ila nina kuku kama 12 kwaajili ya chakula cha nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom