Msaada: Kuku wangu wanapigana sana - nifanye nini waache tabia hii?

Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
2,166
3,827
Habari za majukumu wakuu

Mimi ni mfugaji mchanga nimekuja mbele zenu kuna changamoto ninachopitia kwenye ufugaji wangu wa kuku.

Nina kuku wangu wawili wa kienyeji ni matetea namshukuru Mungu wameweza kupata vifaranga na tatizo ninalopitia ni hawa kuku wangu wametokea kutokuelewana yaani wanapigana sana, toka nilipowaleta walikuwa wakipigana sana nikajua labda kutokana nimewachukua sehemu mbili tofauti nikajipa moyo wanaelewana badae, lakini hali imekuwa ikiendelea mpaka hivi leo naomba MSAADA.

Je, tatizo ni nini au nifanye nini ili waache tabia hii?
 
Mkuu; Una muda gani na hao kuku 2 ?Je, kama wote ni mitetea tafuta jogoo umweke nao awahamulie. Labda nikujuze kidogo kuhusu tabia za kuku. Wanapokutana kuku wengi au wachache e.g. 2, kwanza ni sharti kieleweke.Yupi ni yupi katika kundi;yaani Wanajipanga kitu kinaitwa Hierachy Order. Hili wanalifanya kwa kupigana na hatimaye wakishafahamiana ni yupi mbabe wa kwanza hadi wa mwisho(Mnyonge kuliko wote) huacha mapigano inabaki ni ile ya kudonoana kidogo-kidogo tu na ni kawaida.
Pili; inapotokea nafasi wanayoishi ni finyu, basi huwa wanagombea nafasi kwa kupigana mpaka yule mnyonge a give up na kukaa kwenye kona mbali.
Tatu; inapokuwa chakula hakitoshi kuku hupigania chakula na hapo ugomvi
huzuka.
Nne; kuku wa kienyeji(Indigenous breeds) ni hulka yao kuwa wakali na hupigana sana ndo maana kuku wa kienyeji akiwa na watoto hata wewe atakugonga😂
Tano; Kuku wa kienyeji hawajazoea kuwekwa kizuizini( to be kept in Captivity). Kwa hiyo kama unwafungia kwenye banda wakati huko uliko wachukua walikuwa wanafugwa Huria hiyo inawapelekea kupigana hovyo.
Sita; Kukosa cha kufanya(to be Idle) kuku wakikosa cha kufanya watajitafutia wenyewe cha kufanya. Na kilicho cha kirahisi ni Kupigana.
Kwa hiyo hebu jaribu kurekebisha saizi ya chumba, wape chakula cha kutosha na majani laini mabichi e.g michicha, figili, Mchunga, n.k. uone kama kutakuwepo nafuu. Aidha punguza midomo yao ili kuepusha kusababisha vidonda wanapo pigana.
Endelea kupokea Ushauri kutoka kwa Wataalam husika asante.🙏
 
Namshukuru sana mkuu ushauri wako nitaufanyia kazi

Similar Discussions

Back
Top Bottom