Msaada: Kujiunga rasmi na CCM

Wajumbe wa nyumba kumi niwafanyakazi wa serikali sio chama mkuu..labda niulize ofisi zao hapa nilipo
Sasa ulikua unasubiri nn kama ulikua uanjua ofisi zilipo, au umeambiwa huku kuna kadi za bure
 
Wajumbe wa nyumba kumi niwafanyakazi wa serikali sio chama mkuu..labda niulize ofisi zao hapa nilipo
Sasa ulikua unasubiri nn kama ulikua uanjua ofisi zilipo, au umeambiwa huku kuna kadi za bure
 
Hiki chama kina ushawishi mkubwa sana kwa wale wapigaji. Trust me
 
Huyu yawezekana ni mdogo wake DEO KISANDU amekuja kwa ID nyingine
 
Uko vizuri Kada! Hongera.
Hivi katibana kanuni mpya za CCM zimesha printiwa?!
 
Hapa shida ni nini hasa ...ulitakaje kwa mfano. siamini unachokiamini lazima ukubali utofauti wetu.
Hapana mkuu una haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa ila pia sisi wengine lazma tushangae maana chama ambacho kimetuletea umaskini na uchumi mbaya kwa miaka 50 ya utawala wake na kimeshindwa uongozi ndio unatala kuhamia huko!!!! Kaz kwelikwlei
 
Sikuwezi aisee: Kuna wajumbe wa nyumba kumi kwenye mitaa na hao unaowazungumzia wajume wa mashina wa nyumba kumi
Mjumbe wa shina au Balozi anatokana na chama chochote cha siasa kilicho sajiliwa,ingawa awali vyama vya upinzani havikuwa na huu utaratibu,kwa Chadema wameshaanza nao kuwa na hawa watu muhimu mno kwa ujenzi wa chama wajumbe wa mashina (Mabalozi wa Nyumba Kumi) sinauhakika na vyama vingine.


Pia kuna wajunbe wa Serikali za Mitaa nadhani ndio hawa unao wazungumzia,wewe hawa huwa watano tu ndani ya kila Ofisi ya aserikali za Mitaa,nao huchaguliwa na wananchi wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hutokea kwenye vyama vya siasa kwamaana ya kwamba huwezi kugombea Ujumbe wa Serikali za Mitaa bila kudhaminiwa na chama cha siasa ni kama vile tunavyo waona waheshimiwa Wabunge.

Wajumbe hawa wa Serikali za Mitaa hutenda kama washauri wa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa hawa wamo kwenye system ya Serikali.
Na wakati huu wa muundo wa vyama vingi vya siasa huwa ni mchanganyiko wa Itikadi.
Na hawa huwa hawaruhusiwi kujihusisha kabisa na masuala ya siasa ndani ya Ofisi ya Serikali za Mitaa.
 
Kachukue kadi kibiti, unapewa na uenyekiti kabisaaa!!!
 
kugombea uongozi ni baada ya miaka mitanotangu ulipo jiunga.
 
Ccm oyeee,karibu sana kada kwenye chama cha wazalendo harisi wa nchi hii,chama kilicho asisiwa na Hayati Baba wa Taifa hili,chama cha ukombozi wa Afrika,chama kinacho amini kila binadamu ni sawa na anayo haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa,chama chenye kupigania maslai ya kila mtanzania,Chama kinacho pigana kutokomeza maadui watatu wa Taifa hili ambao ni,
1.UMASKINI
2.UJINGA
3.MARADHI.
Hakika umefanya maamuzi sahihi ya kuwa mzalendo wa Taifa lako,wewe ni mtu huru sasa.
 
mm siamini kama chama kinaweza kuleta umaskini nasema tena siamini na uchumi mbaya sio wa chama na hauletwi na chama umaskini ni attitude zenu na utayari wa kufanya kazi hamna taifa limepata maendeleo kwa kuwa na watu kila kukicha wanashinda kwenye magenge ya kahawa
 
Be consistent with what you try to argue. Naheshimu uzoefu wako kwenye chama lakini mkanganyiko huu unatia shaka
 
Kwa Chadema sasa kila anayeachia ngazi hata kama ameyafanya maovu kiasi gani akiwa ccm kwao ni shujaa wao.Leo hii mnamwona kinana ni shujaa kweli? Mnamwona Mecky Sadik ni shujaa kweli Chadema mko serious mna nia ya dhati na mnaitakia mema nchi hii?
kama walivyo kuwa wema wakati mko nao ccm ndivyo hivyo hivyo watakuwa wema wakija upinzani na uadui utaamia kwenu sawa eeeh
 
Be consistent with what you try to argue. Naheshimu uzoefu wako kwenye chama lakini mkanganyiko huu unatia shaka
Kaka usiwe mzito kiasi hicho bwana,mi nimejaribu kukuelewesha kwasabb ulisema unataka kujiunga na chama nikakupa maelekezo lkn bado unaongelea wajumbe sijui wa chana sijui wa serikali.
Ndipo nikajaribu kukuainishia aina hizo za Wajumbe yaani wajumbe "Mabalozi" wa ndani ya chama na wajumbe wa Serikali za Mitaa hawa hawaitwi Mabalozi bali "Wajumbe wa Serikali za Mitaa" sasa ni jukumu lako hapo kujiongeza ili uelewe nini unataka na utakipata wapi.
Lakini kutokana na haya unayo andika nahisi huko serious au hujijui mwenyewe unataka nini hasa.
Binafsi nimejitahidi kukuelewesha hapo ndo uwezo wangu ulipo ishia.
Pole sana mkuu.
 
Nenda ofisi za CCM Kibiti wana kadi za kumwaga ikiwezekana na cheo unapata siku hiyo hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…