MSAADA KUHUSU ZAWADI ZA VPL

msebia

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
469
357
Nianze kwa kuwapongeza washindi wa ligi yetu ya mpira hapa Tanzania bara Dar Young Africans, pia pongezi ziende kwa vilabu vyote shiriki na shindani katika ligi hii.
Siku ya jana tumeona zawadi zikitolewa kwa vilabu vinne vilivyoingia kwenye nne bora yaani Yanga, Simba, Kagera na Azam na zawadi zao zilikuwa kama ifuatavyo;
Yanga 84m
Simba 42m
Kagera. 30m
Azam. 20m

Swali langu ni
1. Ni vigezo gani vinatumika kuweka tofauti ya zawadi kati ya washindi.
2. Je ni timu zote shiriki hupewa zawadi baada ya ligi kuisha ama huishia kupata gawiwo la vifaa na pesa ya mzamini kwa ajili ya kuendesha timu wakati wa ligi tuu

Nikifanya mrejeo kwenye ligi ya uingereza japo sisemi tuwaige, zawadi kwao hutolewa kwa vilabu vyote shiriki kwenye ligi kwa msimu husika na zawadi hizo ni fedha ambazo huzidiana kwa tofauti ya £1.9m kwa kila nafasi.
Mfano
Chelsea. £38.0 m
Totnhm. £36.1m
Man c. £34.2m
Liverpool. £32.3m

Karibuni wakuu
 
Kabla ya wajuvi kuja, najaribu kuangalia tu tofauti iliyopo kati ya Uingereza na Tanzania. Tuko nyuma sana., ni zaidi ya mno!

Bingwa England = Bilioni 110
Bingwa Tanganyika = Milioni 84

Tofauti ya zawadi ni mara 1,311! Kwa kweli dunia haiko fair kabisa. Sitaki kuamini kiwango cha uchezaji wa ligi hizi ni tofauti ya zaidi ya mara 1,311
 
Back
Top Bottom