Msaada kuhusu usajili wa kampuni, BRELA wanatukatisha tamaa katika hili

gudby

Member
Joined
Dec 5, 2013
Posts
11
Reaction score
2
Wadau naomba msaada, sisi ni vijana tumemaliza chuo na tumeamua kujikomboa kiuchumi kwa kuamua kuanzisha company yetu binafsi ya usambazaji wa vitu mbalimbali especially stationaries.

Tukaenda BRELA kwa ajili ya usajili wakatuambia tutafute memorandam, article of association na mwanasheria wetu tukavifanya vyote hivyo na tukawapelekea wakaikubali ile memorandum & article of association mwanasheria wetu akagonga mihuli pamoja na sign yake ktk zile document ili turudishe BRELA kwa ajili ya process nyingine tukarudisha wakatuambia tu download form kwenye mtandao wao tukafanya hivyo na kuijaza then tukawarudishia wakatuambia tuacheni then tutapitia ili kujua kuwa mtalipia sh ngap then mlipe ili tuwape certificate yenu.

Ajabu toka tujibiwe hivyo ni week ya 3 sasa kila tukiwafuata wanatuambia bado tunafanyia kazi na siku moja tuliwaganda sana wakatuambia mnatakiwa mlipie laki 8 kwa hi company yenu, tukawauliza kivipi wakasema basi njooni kesho tutawamalizia lakini mpaka leo tunapigwa tunazungushwa.
 
Mbona ndio zao pale! Ila ukiwapa kama shilingi elfu 50 cku mbili tu wanakupa hiyo certificate na usipo angalia utasota sana.KWELI ALIYETUFIKISHA HAPA ALANIWE.
 
mimi nimepata certificate ya kampuni yangu Jan 21 ....bila longo longo wala Urasimu
 
Mbona ndio zao pale! Ila ukiwapa kama shilingi elfu 50 cku mbili tu wanakupa hiyo certificate na usipo angalia utasota sana.KWELI ALIYETUFIKISHA HAPA ALANIWE.

50 nyingi mbona,30 tu unamuita mmoja pale mwambie muongee kuitu uzima akusaidie,ndani ya wiki tu ishakamilika
 
Malipo halali ambayo unapewa receipt ya serikali inategemeana na idadi ya shares. kwa uzoefu wangu wa kusajiri kampuni pale brela. Wadau wengi unalipa around laki 3 mpaka 5. Hayo ni malipo halali kabisa. Na kwakuwa mnamwanasheria aliyegonga mihuri hizo document zenu, mwambieni awasaidie. Rushwa ni hiari yako kutoa. Binafsi sishauri utoe rushwa kwenye kusajiri kampuni maana kuna msululu bado mpaka uje uje uanze kazi.
Ukitoka brela uende TRA kwaajili ya TIN then uende halmashauri kwaajili ya leseni huku nako kuna malipo halali ya serikali, mtafute ofisi na kuilipia halafu mtafute furnitue za kuanzia, mlipie maji, umeme huenda mkatakiwa kununua luku yenu. Kijana wa usafi, mlinzi.
Kama mpaka jumanne hamjapata unPM

Na mwisho niwapongeze kwa kuchukua maamuzi magumu ambayo hamtajutia as long as hamsalitiani na hamna mwenye haraka kuliko wenzake. Kila la kheri.
 
Tokeapo rushwa ni hiari yako ni uamuzi wako ile nenda rudi kwa miezi 2 na kutoa elfu 30 ndani ya siku mbili ukapata hicho cheti!na hata huko tra,manispaa upende usipende tu lazima utaachia.mfano kwenye Tin huwa ni bure sawa ngoma inakuja pale kwenye makadilio ya kodi ndio huyo mkadiliaji mtaongea vizuri ili akupe makadilio ya chini,utatoka hapo utakwenda halmashauri kifuatilia leseni itakutana na watu waidara ya afya ili wakipitishie hiyo form watakwambia lazima twende kukagua eneo husika!!!we hii nchi ilipofikia utaonekana kama ----- fulani hivi useme una taka haki bin haki labda kama huna haraka na kitu chako wakikwambia njoo mwezi wa nne sawa tu,lakini kama una kimbizana na muda utakubali tu kugeukia kibla.
 
Mbona ndio zao pale! Ila ukiwapa kama shilingi elfu 50 cku mbili tu wanakupa hiyo certificate na usipo angalia utasota sana.KWELI ALIYETUFIKISHA HAPA ALANIWE.
Yaani hawa jamaa ni balaa nilisota pale wiki mbili wakaja wazungu siku moja tu wakamalza kusajili na wakasindikizwa na wakubwa huku wakicheka.Hawa wana pepo wa ubaguzi kwa waafrika wenzanzao.Kwa kweli wanakatisha tamaa!!Na ni hatari kwa vijana wanaotaka kujikwamua.
 
Mtafuteni dada mmoja anaitwa Rehema Kitambi,ni mzito pale brela ..Yuko very kind,friendly & helpful atawasaidia fasta,ni mdada mwenye moyo wa kipekee na mkarimu..Muwe serious ilimradi
 
Yah we are serious ktk hili ndugu kama una no ya huyo dada unaweza ukansaidia kwa ku ni PM hiyo no yk ili tuweze fanya naye mazungumzo.
 
Siwezi kukupa namba yake sababu ni kwamba sikufahamu,pole..Ila kama unaweza nenda pale omba appointment nae ukisema una ishu binafsi umeagizwa au vp wakikuruhusu ushapeta wewe ..
 
Malipo halali ambayo unapewa receipt ya serikali inategemeana na idadi ya shares. kwa uzoefu wangu wa kusajiri kampuni pale brela. Wadau wengi unalipa around laki 3 mpaka 5. Hayo ni malipo halali kabisa. Na kwakuwa mnamwanasheria aliyegonga mihuri hizo document zenu, mwambieni awasaidie. Rushwa ni hiari yako kutoa. Binafsi sishauri utoe rushwa kwenye kusajiri kampuni maana kuna msululu bado mpaka uje uje uanze kazi.
Ukitoka brela uende TRA kwaajili ya TIN then uende halmashauri kwaajili ya leseni huku nako kuna malipo halali ya serikali, mtafute ofisi na kuilipia halafu mtafute furnitue za kuanzia, mlipie maji, umeme huenda mkatakiwa kununua luku yenu. Kijana wa usafi, mlinzi.
Kama mpaka jumanne hamjapata unPM

Na mwisho niwapongeze kwa kuchukua maamuzi magumu ambayo hamtajutia as long as hamsalitiani na hamna mwenye haraka kuliko wenzake. Kila la kheri.

Ndugu nashukuru sana kwa maneno yako mazuri ya kututia moyo ntaku PM ndugu endapo kama tutakuwa hatujapata mpk jumanne.
 
Siwezi kukupa namba yake sababu ni kwamba sikufahamu,pole..Ila kama unaweza nenda pale omba appointment nae ukisema una ishu binafsi umeagizwa au vp wakikuruhusu ushapeta wewe ..

Ahsante ndg I will try to work on that.
 
Nyie mmeenda mbali sana! Hapo chini Brela jamaa unaowaonaga hapo ni vishoka na ndio kazi zao nyie mmenda Front sana, ni sawa na wale jamaa wanaokaaga ofisi za TRA unawapa kazi na kitu kidogo wanamaliza kazi yako fasta. GOD BLESS TANZANIA AND NO OTHER COUNTRY ELSE!
 
Back
Top Bottom