Msaada kuhusu ubora,uimara wa nissan x-trail

Msaada kuhusu ubora,uimara wa nissan x-trail

iparamasa

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
13,437
Reaction score
14,934
jamani hii gari ninaipenda,nataka kujua uimara wake na ubora kwa wajuzi kabla sijainunua,please,an advice
 
Xtrail gari nzuri asikwambie mtu.....spare zake ziko ila ghali kuliko Toyota.Gari nzuri,gari imara haina matatizo kabisa kama ukizingatia SERVICE kwa wakati....Ingia SBT uagize mwenyewe.
 
Ni gari nzuri sana, lakini singatia service kwa wakati, maana spare zake ni ghali, lakini ukifunga unasahau!
 
gari zuri na imara, vipuri vyake pia imara....
 
Xtrail gari nzuri asikwambie mtu.....spare zake ziko ila ghali kuliko Toyota.Gari nzuri,gari imara haina matatizo kabisa kama ukizingatia SERVICE kwa wakati....Ingia SBT uagize mwenyewe.

Mdanganye tuu mwenzio
 
Naongezea -

Nunua mpya au iwe kwenye hali nzuri
 
Hilo ni janga la taifa, kwanza spare zake ni very expensive, na gari haina uwezo wa kumudu mikimiki, nakushauri bora utafute rav4, nina ushahidi na ninachokisema
 
Ni magari ambayo bei yake kwa ujumla iko chini ukilinganisha na Toyota. Spare zake nadhani "not easily available" well, hii inategemea sehemu uliyopo. Engine yake haikutengenezwa kwa cast iron bali imetengenezwa kwa alminium. Na hii wataalamu wanasema ndo maana bei yake iko chini!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Hilo ni janga la taifa, kwanza spare zake ni very expensive, na gari haina uwezo wa kumudu mikimiki, nakushauri bora utafute rav4, nina ushahidi na ninachokisema
si kweli ni gari imara iko poa halafu ni4wd mkuu
 
Mbali na michango ya hapa pia napenda kukuambia jitahidi uwe na chaguo lako kwa kitu unachokipenda, mfano mimi naweza kukuambia gari fulani inafaa/ninayoipenda mimi, mwingine nae akakuambia inayomfaa yeye au naweza sema anayoipenda yeye.

Pokea michango yote ya hapa kisha na wewe muhusika mkuu uwe na maamuzi ya mwisho kwa lugha nyingine maamuzi binafsi
 
Hii gari siitamani tena nakumbuka ilashawahi kuniburstia tairi dah acha kabisa halafu speed kibati,nilifunga tairi za China sisahauuu...all in all gari iko poa zingatia service I hope you will enjoy it.
 
Xtrail sio gari nzuri,zinaharibika sana injini. Tatizo lao kubwa ni injini,cylinder head zake zinawahi kuharibika na kuchanganya. Sikushauri mkuu ununue xtrail. Nunua gari nyingine ila xtrail utakuja nambia.
 
Kwa ujumla nissan ni.nzuri kama ni mpya ila used utalia si muda mrefu. Ni mzuri sana miguuni ila injin bomu. Wengi unaowaona wamejaa kwenye hizo gari wameweka injini za.rav4. Kama utakubaliana na kuweka injini nyingine nunua. Injini bomu sana kaka ndio maana bei zake down
 
Hilo ni janga la taifa, kwanza spare zake ni very expensive, na gari haina uwezo wa kumudu mikimiki, nakushauri bora utafute rav4, nina ushahidi na ninachokisema

MKUU acha kukalili wewe nani kakudanganya .
ushakremishwa na mafundi wako wauchochoroni kuwa engine ya RAV 4 3S ni roho ya paka.

ushawahi miliki gari??
nani kakwambia kuwa Nissan gari mbovu??
katika gari ambayo inakubalika na haina SPEA fake kama magari ya Europe basi kwa Asian car mm kwangu naipa best..
hakunaga SPEA za magumashi ukifunga unasahau MKUU.
tatizo lenu mnapenda vitu vya bei chee
 
Back
Top Bottom