Msaada kuhusu Toyota Coaster

Msaada kuhusu Toyota Coaster

Mkanganyiko

Member
Joined
Feb 3, 2014
Posts
34
Reaction score
11
Habari zetu wana jamvi...naomba kujua bei ya Toyota Coaster hapa dar kwenye show room. Pia endapo nitakuwa na pesa pungufu ya kununulia inawezekana kupewa gari halafu ukalipa kidogo kidogo hadi deni litakapoisha? Mwisho napenda kujua ni wapi naweza kupata coaster kwa njia ya kulipa nusu ya hela halafu tukaendelea kulipana.
Nawasilisha
 
Mkuu huna haja ya kununua mpya unless umepetaa tender ya Hotel au ofisini.
Maana kipindi hiki Dar zinauzwa bei ya chini sana kwa wamiliki wanaosoma alama za nyakati.
Bei ya Show room sio chini ya 45m long na 40 - 35 short.Hii ni kwa kuhangaika lakini,maana zipo hadi za 60m.
 
lakini huyu jamaa anaonyesha anataka kukopa ili alipe taratibu,haonyeshi kuwa anataka mpya au iliyotumika
 
Wakuu ninataka kuchukua hata used kibongo bongo je kwa experience zenu naweza kupata kwa bei gani iliyosimama vizuri?
 
Used kaka itakutesa,utaliwa kwa Dar.
Coaster nyingi Dar Engine sio zake au unakuta imeishafunguliwa.
Subiri Darts waanze ujiande na 20m kupata Coaster ya kawaida
 
Used kaka itakutesa,utaliwa kwa Dar.
Coaster nyingi Dar Engine sio zake au unakuta imeishafunguliwa.
Subiri Darts waanze ujiande na 20m kupata Coaster ya kawaida
Wazo zuri kabisa,wauzaji bongo hawasemi tatizo la gari utawasikia hari haiaguswa injini na huku hana service card ni kituko bana straight Japan suluhisho
 
Back
Top Bottom