Kwa uzoefu wangu mdogo Elimu ya South Africa ina value kwenye Soko lao la ajira zaidi, unaweza kuomba kazi ukiwa na degree yako ya Tanzania usifanikiwe na mwenzio mwenye Certificate may be ya Course ya miezi 6 ambayo kaipata huko huko ndani ya nchi yao akapata ajira, fulsa za ajira zipo na Wa South Africa wengi hawataki kwenda shule ama kufanya kazi, soko la ajira limetekwa na Wasomi kutoka Zimbabwe.
Kuhusu gharama za maisha kuna utofauti na Tanzania, mfano kupanga chumba kimoja bei ya chini inaanzia R500 mpaka R800, na hii ni kwa sehemu ambazo ni Uswazi, kwa R1000 mpaka R1500 unapanga nyumba nzima Uswazi (but pandemic hizo usalama ni MDOGO).
pia unaweza kupanga nyumba kwa R2000 na kuendelea sehemu ambazo kidogo kuna ustaarabu.
Hostel zipo zinatofautiana kuanzia R100 kwa week na kuendelea.
Kuhusu chakula kama unakula kwenye hotel za mtaani utapata chakula kwa R30 na kuendelea, kifupi ukiwa na R100 unakula kwa siku nzima, kama utapika mwenyewe gharama ni ndogo zaidi, mfano kuku 1kg inauzwa R15, mkate R5, bia R12 kwa ufupi maisha ni rahisi kama chanzo chako cha pesa kipo South Africa.
Tatizo kubwa la South Africa hakuna usalama hata kidogo, hafu ni mbaya wakijua kuwa ni mgeni!
sijui kama ntakua nimesaidia kupata picha.
NB: R1 sawa na T'sh 150.