Msaada kuhusu second round

diuretic

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
355
Reaction score
618
Habari za siku wakuu. Je kwa matokeo haya kwa PCM nilipata CCC. Nilikosa 1st round sasa nimeapply second round computer science udsm, computer science IFM, Geoinformatics Ardhi na IT IFM. Wakuu kwa machaguo haya naweza pata au nikakosa. Nipo open kwa maoni na ushauri wenu.
 
Tatizo hujui kuchagua vyuo. Unachangua vyuo vyenye competition kubwa sana maana kila mtu anajaza UDSM, IFM, ARDHI na MZUMBE.

Tafuta na vyuo vingine ujaze. Tofauti na hivyo
Lasivyo utaisoma namba
 
Hapo jiandae na 3rd round

Tatizo watoto mnataka kujazana daresalama wote ili hali vyuo vimetapakaa tanzania nzima
 
Hapo jiandae na 3rd round

Tatizo watoto mnataka kujazana daresalama wote ili hali vyuo vimetapakaa tanzania nzima
Sawa mkuu ntaongeza nafasi moja kozi isiyo na ushindani. Ila ufaulu wangu sio mbaya sana nna division 1 ya 9 kwa PCM
 
Wenye division moja ni wengi tatizo ni competition omba na vyuo vingine kama RUCU INA kozi baadhi unazo zitaka.waweza kosa chuo dispute having ccc
 
Piga moyo konde na Mungu atakusaidia, hivi 2nd round inaonesha na idadi ya mlio-apply maana hii ingekuwezesha kujua competition ipo vipi. ALL THE BEST!
 
Piga moyo konde na Mungu atakusaidia, hivi 2nd round inaonesha na idadi ya mlio-apply maana hii ingekuwezesha kujua competition ipo vipi. ALL THE BEST!
Hawaoneshi mkuu unaona tu nafasi zilizobaki.
 
Naombeni msaada wadau, kuna dogo kakosa first selection na kaomba upya kama ifuatavyo
1.RUCU-Baed(remaining capacity 22)
2.SAUT(Arusha)-Baed(remaining capacity 233)
3.UDOM-Bachelor of arts in english(capacity 24)
4.MAKUMIRA(Arusha)-Baed(capacity 102)
5.KIU-Baed (capacity371)

COMB_ (HGL)
Matokeo (2 ya 11)

Vipi hapo anawezapata chuo, au afanye nn ili awe n uhakika wa kupata chuo.?
ushauri tafadhari.
 
Kwa ufaulu huo na choice alizofanya wala asihangaike naimani lazima atapata
 
Mkuu acha tu nimechanganyikiwa kukosa 1st round sikutegemea ila ndo hivyo.
Unapofanya application ni lazima ujifanyie tathmini ya uwezo wa kushindana na waombaji wengine kwa kuzingatia:
1. Ufaulu wako
2. Kiasi cha nafasi (capacity) kwenye kozi na chuo husika ulichochagua
3. Idadi ya competitors waliopo wakati unachagua na siku moja kabla ya dirisha la maombi kufungwa.
Nafasi zinaweza kuwa ni nyingi lakini washindani ni wengi zaidi. Na nafasi zinaweza kuwa kidogo lakini na washindani ni kidogo zaidi.
Hivyo wingi wa nafasi ulinganishwe na wingi wa washindani katika kufanya maamuzi
Tathmini hiyo itakuongoza kuhama chuo kwa kozi hiyo hiyo au kubadili kozi na chuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…