Msaada kuhusu pump ya kumwagilia

Msaada kuhusu pump ya kumwagilia

g4cool

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
431
Reaction score
211
Habari zenu wakuu, nimechimba kisima cha mkono cha futi kama 35 hv (10.666 meter) na nataka ninunue mashine kwa ajili ya kumwagilia, swali langu ni je
1. Nikichukua zile za kudumbukiza kwenye maji (submersible) ya 0.5hp na jenerator la 1 hp na mpira wa nchi moja nitaweza kupata maji ya kutosha ya kumwagilia heka 2?? (Sitaki kuyapeleka kwenye tanki, yaani nikiyatoa kwenye kisima ni moja kwa moja shambani) AU
2. Nikichukua hizi mashine za kawaida sijui kingmax au ingco nk zinazotumika kumwagilia toka kwenye mito au mabwawa zitanifaa?? Maana nyingi naona suction yake zinaishia futi 26 ambayo ni kama mita 8?????
 
Surface pump/booster ndio hizo unazoona zinakaa juu maji yanakua chini.zinauwezo wa kusukuma maji umbali mrefu lakini si kunyonya.Hivo kama maji yako karibu kama maji ya ziwa,mto au kisima kifupi si zaidi ya mita saba. Zinafanya kazi vizuri.hizi ni pump ambazo zimefungwa na engine au motor na hazilowekwi ndani ya maji.
Submersible pump, hii ni maalum kwa visima virefu kuanzia mita nane kwenda chini.zina uwezo mzuri wa kupandisha maji kutoka chini Kuja juu. Total head. Hii unahesabu kutoka pump ilipo hadi kwenye tank vertical. Ni vizuri kutumia submersible pump kwa kisima maana hata maji yakipungua itasukuma inashauriwa uweke tank,ili ifanye kazi moja yaani kupandisha,na si kuipa na kazi ya pili kusafirisha hayo maji. Kwa ufupi ni hayo
 
Ahsante mkuu kwa maelezo mazuri
 
Hata mimi nashauri utumie tank. Tatizo lingine, usipotumia tank, utapata hasara maji yatakuwa yanapotea sana kwa mfumo wa kumwagilia moja kwa moja. Ukipandisha kwenye tank, utakuwa unamwagilia kwa muda unaotaka wewe, na kwa kiasi cha maji unachotaka wewe. Unaweza kujaza tank, lakini ukamwagilia kwa kutumia nusu tank, alafu ukasitisha ukaendelea kesho yake.
Hata wale wanaotumia pampu za kutoa maji moja kwa moja kutoka mtoni hadi shambani wanapoteza maji mengi sana na pia mafuta ... Akili kichwani
 
MKOMBOZI WATER PUMP Inaundwa na wazalendo.Ni PAMPU ya mkono.Fuatana nami. 0765793347 Tupo Mbeya jiji.Tumeweza
 
Screenshot_2018-02-21-18-27-32.png
Screenshot_2018-03-20-18-27-53.png
Screenshot_2018-03-18-13-13-06.png
 
Back
Top Bottom