Msaada kuhusu madini

Msaada kuhusu madini

uroto

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
447
Reaction score
233
Habari wana jukwaa

Mimi ni mkazi wa Dodoma,maeneo ya mpwapwa,kuna ndugu yangu aliomba shamba awe analima,

Nilimpatia likiwa ni pori,amelisafisha ila aliokota mawe mawili ambayo anadai ni kama madini,alipoyapeleka sehemu husika,waliomba waje wapime,walipopima wakasema eneo hilo lina madini aina 2 ambayo yanahitajika sana nchini China,mojawapo ya dini hilo,ni gold shine

Msaada wenu sana jamvi,nifanye mini ili nifaidike na fursa hii,maana usawa mgumu alafu Nimebahatika kupata ardhi yenye utajiri

Nb:Shamba bado ni langu,ndugu aliomba atumie kipindi hiki cha mvua tu
 
Weka picha za hayo madini, nikijiridhisha nitakusaidia Kila kitu, wewe hutatoa hata Senti tano
 
Bangi ikikutwa shambani kwako ni yako na tunakushtaki.
Madini yakipatikana shambani kwako ni mali ya mwekezaji anaweza kua mzungu au mchina na wewe hapo unatakiwa uhame haraka uwaachie wawekezaji. Wakiyamaliza utarudishiwa shamba lako uanze kufukia mashimo na makemikali
 
Mkuu, toa haraka taarifa Serikalini. Madini ni mali ya Serikali. Usidanganywe kuanza kuchimba, utatenda jinai. Ukitoa taarifa, kutakuwa na utaratibu maalum wa kukufidia eneo lako.
 
Atafidiwa kama laki mbili tati halafu mchina anapewa achukue utajiri bwelele. Pia akikutwa na hayo madini. Imekula kwake.
 
Habari wana jukwaa

Mimi ni mkazi wa Dodoma,maeneo ya mpwapwa,kuna ndugu yangu aliomba shamba awe analima,

Nilimpatia likiwa ni pori,amelisafisha ila aliokota mawe mawili ambayo anadai ni kama madini,alipoyapeleka sehemu husika,waliomba waje wapime,walipopima wakasema eneo hilo lina madini aina 2 ambayo yanahitajika sana nchini China,mojawapo ya dini hilo,ni gold shine

Msaada wenu sana jamvi,nifanye mini ili nifaidike na fursa hii,maana usawa mgumu alafu Nimebahatika kupata ardhi yenye utajiri

Nb:Shamba bado ni langu,ndugu aliomba atumie kipindi hiki cha mvua tu
Ulipata suluhisho? Tushirikishane uzoefu, tafadhali!
 
Back
Top Bottom