Msaada kuhusu kuvuta maji dawasco

Anko Elly

Member
Feb 22, 2017
69
70
Waheshimiwa napenda kuwasalimu Asallaam alleikhu na bwana asifiwe, matumaini yangu kuwa hamjambo na poleni na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini kwetu Tanzania, halikadhalika nawapa pole ndugu zetu wa Tanzania Visiwani.

Wahenga walisema kwamba kwenye wengi kuna mengi, nahitaji mnieleweshe hatua za kupitia ili niweze kuvuta maji ya bomba ya Dawasco ambayo sio maji chumvi, ninapoishi ni kama umbali wa mita 15 kutoka kwa jirani yangu mwenye bomba.

Je, hatua za kufanya nazotakiwa nianze nazo ni zipi? kingine gharama inaweza ika-range kwenye kiasi gani? process nzima inaweza ikachukua takribani siku ngapi na kufungiwa mita?samahani kwa kuwachosha kwa maswali, Wajuvi wa mambo karibuni.

Nawasilisha
 
Hatua unazopaswa kuchukua ni wewe kwenda ofisi za DAWASCO uwaelezee shida yako na watakusaidia...Utahudumiwa vizuri tu, hawana shida ukifuata utaratibu mkuu
 
Back
Top Bottom