Msaada kuhusu kupima DNA

Msaada kuhusu kupima DNA

Mahunda Jr

Member
Joined
Apr 5, 2020
Posts
76
Reaction score
108
Habari,

Nina mtoto nimemlea kwa takriban miaka miwili hivi, nampenda sana uyu mtoto na ndo mtoto pekee nilienae kwa sasa ila njia ya mama yake na yangu zimeenda tofauti na kila mtu na maisha yake.

Kwa muda mrefu kidogo mtoto nlimpeleka kulelewa na bibi mzaa mama yake tena akiwa ananyonya baada ya mama yake kunitelekezea mtoto.

Nlimpa yule mama huduma zote za mtoto ikiwo bill ya maziwa na mahitaj mengine. Mtoto akaanza kusimama na kutembea akiwa kwa bibi nami nilimhudumia vizur tu.

Mama yake akaanza maneno kuwa mtoto sio wangu, akarudia na kurudia na kila nlipowashirikisha wazaz wake waliniambia nimblock kwakuwa ni hasira za kuwa mbali na mtoto kwakuwa japo alikutelekezea ila alipojua umemleta hapa nyumbani alimtaka mtoto ila tukamkatalia kwakuwa tumeshamwachisha nyonyo na kwamba mtoto aliletwa kwa maandishi kutoka serikal ya mtaa kwahiyo hawezi kutoka tena atakaa pale.

Basi nlipoambia ni hasira nkapuuza na kupuuza na kupuuza kila aliponitamkia hayo maneno.

Uvumilivu una kikomo, na ulikoma pale aliponitajia baba wa mtoto kwa jina kabisa na ni mwanaume ambae alishakuwa nae kimahusiano. Nikaacha kuhudumia vikaanza vikao visivyo na mwisho na visivyoeleweka na visivyo na suluhu. Nimesitisha huduma tangu mwez wa tisa.

Najiskia vibaya kutokumhudumia uyu mtoto hasa ikiwa ni wangu, ila ntajiskia vibaya kama ntahudumia mtoto sio wangu.

Naomba kwa anaejua gharama na taratibu za kupima DNA anijulishe mana hili swala ni gumu sana kwangu. Ikiwa gharama ni rafiki basi nikapime.

Asante
 
Ivi embu jiulize utakapopima ukaambiwa sio wako utafanyaje?

Mimi sioni hata haja kupima, maana umemkubali na kumlea toka uchanga wake kwa Imani kuwa mwanao na Damu Yako. Huyo mwanamke asikutoe endelea tu na jukumu Hilo jema ulilolianzisha. Ikibidi Fanya kama uliyemuokota jalalani.

La msingi wamleee, ikifika wakati muafaka, chukua mtoto wako.
 
Hupaswi kuamini chochote kutoka kwa mwanamke aliyemtelekeza mwanae akiwa mchanga.

Kama umeweza kumlea mtoto angali mchanga endelea kufanya hivyo, huenda riziki yako inatoka kwenye baraka za huyo mtoto.

Kama ukifanikiwa kupima na kugundua mtoto sio wako, usimtelekeze. Endelea kumpa huduma hadi atakapokua, Mungu anajua zaidi kwanini alimuweka huyo mtoto katika mikono yako.
 
Ivi embu jiulize utakapopima ukaambiwa sio wako utafanyaje?

Mimi sioni hata haja kupima, maana umemkubali na kumlea toka uchanga wake kwa Imani kuwa mwanao na Damu Yako. Huyo mwanamke asikutoe endelea tu na jukumu Hilo jema ulilolianzisha. Ikibidi Fanya kama uliyemuokota jalalani.

La msingi wamleee, ikifika wakati muafaka, chukua mtoto wako.
Itakuaje ikiwa sio wangu na ntakuwa nimepoteza gharama zangu zaid, na itakuwaje kama baba yake yupo kwel kama mama yake anavosema siku akija kumdai mtoto kila mtu atanigeuka kwakuwa nimeshaambiwa sio wangu nikakaza fuvu
 
Sasa unaumia Kwa kusitisha huduma wakati mama yake alionyesha nia ya kumchukua mtoto na hapo hapo ulipaswa kuruhusu amchukue mtoto Kwa kuwa tayari alianza kusema mtoto si wako huku ukisikilizia, mpambano uendelee kwenu wenyewe pasipo mama mkwe wako kujua kinachoendelea na hata ungesitisha huduma mtoto akiwa kwa mama yake hata kama atalalamika ataonekana yeye ndio mkorofi maana mtoto alipokuwa kwa bibi yake ulikuwa unatoa huduma

Kumbuka kule ulikompeleka mtoto ni kwa mama yake mzazi na lazima atam-protect mwanae lakini pia atakutia moyo ili mradi mambo yapite

Sasa wewe ndo umeonekana huna busara Kwa kusitisha huduma na umebaki kuumia na huko huyo mzazi mwenzako anakukaanga sasa hivi kwa mama yake kwamba wewe ni mkorofi anatoa na mfano wa kusitisha huduma na ukute amekukana kwamba hajakuambia sio mwanao.
 
Wewe ukimuangalia huyo mtoto unaona kuna kipi unachofanana nae? Kama hakuna hiyo ni redflag namba 1.

Kapime DNA bila kujali gharama ni kheri ujue kwamba si damu yako bado mapema, maana unaweza kujikita ktk matunzo na kubania uzazi mwingine kutokana na majukumu uliyonayo muda ukaenda bila mtoto wako wa damu..

Ukishajua kuwa SI wako, usikatishe huduma bali upunguze huduma..

Dunia haiko fair wale wanaokupa moyo wa uvumilivu wa kulea mtoto si wako ndio hao hao watakaokucheka kuwa ni bwege. Hakikisha mapema kbs kama ni damu yako.

NB:Mtoto wa kulea ambae unajua si wako ni tofaut na yule ambae unajua ni wako alaf unakuja kuambiwa si wako.
 
Kwakifupi ni kwamba hakuna hasira za muda mrefu namna hiyo. Yaani mtoto awe wako harafu mama yake awe anaimba kila siku kuwa mtoto si wako!!!!!!. Kwakifupi acha hata kupima we amua tu kama unahudumia kama msaada ama unaangalia ustaarabu mwingine. Hapa wameshakuja na kukuambia eti baraka zako ziko kwa huyo mtoto. Hebu waulize kama wameshasaidia hata katoto kamoja ka kwenye mazingira magumu kama wameweza kupata hizo baraka
 
Mkuu hilo mbn simple tu we,piga kimya alafu maji,na,mafuta vitajitenga apo,baadae,ni,swala la,mda,tu na,damu ni,nzito kuliko maziwa mkuu na,kama,ni,wako wala hauna haja yakutumia nguvu kuuuubwa we relax mambo yataji,set yenyewe maana,mtu nitofauti na,kitu,mkuu. na,usiumie,kichwa kwa,jambo,hilo mambo mengine unaacha,tu,asili ifanye kazi yake na,hapo ndipo unapoonekanaga uzito wa,damu. na,usionyeshe sura yakugombania mtu we endelea na,mishe zako,tu.
 
Gharama ya DNA ni Wastani wa 150,000.....!

All in all kila kinachotokea Kwa Binadamu kina sababu.
Ipo sababu Kwa Nini umeachana na huyo Mwanamke.....!
Pia ipo sababu Kwa Nini umeletewa huyo Mtoto na Mungu ili Umtunze...!
Na ipo sababu pia ya huyo mwanamke kwanini atamke maneno hayo. Ashapewa tahadhari na Mungu aloshasema tuishi nao kwa akili. Sasa yeye ashupaze shingo aingie mkenge. Mungu hana huruma na wajinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom