Fahamu kilimo bora cha njegere na jinsi ya kudhibiti wadudu waharibifu

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
804

1601214399454.png

Wadau wanaotaka kujua kuhusu kilimo cha njegere
WAkuu mwenye uzoefu tunaomba tuelekezane juu ya kilimo cha zao hili.
-----
Ndugu zangu naombeni msaada kuhusu kilimo cha njegere, upatikanaji wa mbegu, changamoto zake - magonjwa, madawa, na inahitaji kiasi gani cha mvua, aina ya udongo n.k
----
Wakuu salamu, wataalam wa kilimo naomba mwenye document ya kilimo bora cha njegere maswala muhimu ikiwa ni namna ya kuandaa shamba, msimu mzuri wa kulima, nafasi kati ya mmea na mmea yaani formula ya upandaji, mbolea ya kutumia na mengineyo, asanteni.
----
Naomba msaada kwa mwenye uelewa wa kilimo cha njegere
1. Yapi maeneo sahihi ya ulimaji
2. Upatikanaji wa maeneo husika na garama zake
3. Changamoto za kilimo hiki (faida na hasara)
4. Soko la njegere
5. Wapi au nani naweza mtembelea nikajifunza
6. Jarida, kitabu au blog yeyote ninayoweza pata taarifa sahihi
Na taarifa yeyote utakayoona inanifaa. Tafadhali ninaomba msaada wenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Fahamu kiundani hatua za kulima njegere
Nakusihi kulima kilimo hiki kwa kwa sababu , kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

Mwazoni Njegere zilipatikana mwishoni mwa kipindi cha neolithic era huko Greece, Syria, Turkey na Jordan. Na Egypt, ilipatikana mwanzoni mwa miaka ya ca. 4800–4400 BC eneo la Nile delta, na kutoka ca. 3800–3600 BC Egypt juu. Pia Njegere zilikuwepo huko Georgia millennium ya 5 kabla Yesu hajazaliwa (BC).

Njegere zilikuwepo eneo la Afghanistan ca. 2000 BC, maeneo ya Harappa, Pakistan, na kasikazini-magharibi mwa India mwaka 2250–1750 BC. Katika kipindi cha millennium ya pili BC, hili zao lilionekana katika mto wa Ganges na India kusini na kusambaa duniani.

Hapa nchini Tanzania hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina.

Spishi kadhaa za njegere ni:

1. Njegere kubwa (chickpea)

2. Njegere ya kizungu (common pea)

3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu njegere hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.

Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

HALI YA HEWA:

Kwa tafiti inaonesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

UTAYARISHAJI WA MBEGU

Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

UPANDAJI.

Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.

ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.

iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.

iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

MBOLEA.

Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) njegere hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.

UPALILIAJI

Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya mda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.

Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MAGONJWA & WADUDU

MAGONJWA.

Ascochyta.

Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

Root Rot na Blight disease.(kuoza kwa mizizi na Blingt)

Husababishwa na fangasiA. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .

Kuzuia.

1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.

2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

Downy mildew.

Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.

Dalili: Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na

kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa

unyevunyevu.

Kuzuia: – Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

Fusarium wilt:– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.

Dalili:

1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.

2. Mimea kudumaa.

3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.

Kuzuia: – Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.

Virusi
– Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.

Kuzuia: – Kutumia mbegu zisizo na maradhi.

WADUDU

Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

UVUNAJI

Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.

Michango ya wadau

Hiki kilimo kina changamoto sana hasa kwenye bei unaweza kuta leo gunia elfu 50 afu kesho elfu 20!
Na kuna wakati zari linaweza kukudondokea unakuta unavuna Kila gunia laki moja!
Iringa ndo wanalima sana!

Soko ni kariakoo kama una mzigo mkubwa au unaweza amua kuwauzia wachuuzi ambao wanapeleka huko kariakoo!
Aina za mbegu ipo namba 3 na namba9
Hii namba9 mara nyingi inapandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua kwasababu haiwezi kuhimili mvua kubwa sana!
Ila namba tatu inaweza kuhimili mvua kubwa ndio maana hupandwa miezi ya January na kuendelea!

Ila unaweza panda kiangazi kwa kufanya umwagiliaji ila huwa changamoto ya dawa kwasababu hushambuliwa sana na ukungu, tofauti na ukipanda msimu wa masika huitaji kupiga dawa yoyote!!

Kwa kifupi ni ivo mkuu Ngoja wadau wengine waje wakupe nondo zaidi!
----

Asante kwa kuniita,

Njegere ni jamii ya legumes, huota na kuzaa vzuri ktk nyanda za juu kwenye baridi. Kwa hapa Tz Iringa,Njombe na Mby ndio kwenyewe. Ngoja nipate nondo za kisayansi kasha nitarudi.
 
Tunae
Asante kwa kuniita,

Njegere ni jamii ya legumes, huota na kuzaa vzuri ktk nyanda za juu kwenye baridi. Kwa hapa Tz Iringa,Njombe na Mby ndio kwenyewe. Ngoja nipate nondo za kisayansi kasha nitarudi.
ndelea kusubiri..... :)
 
Ndugu zangu naombeni msaada kuhusu kilimo cha njegere, upatikanaji wa mbegu, changamoto zake - magonjwa, madawa, na inahitaji kiasi gani cha mvua, aina ya udongo n.k
 
Wakuu salamu, wataalam wa kilimo naomba mwenye document ya kilimo bora cha njegere maswala muhimu ikiwa ni namna ya kuandaa shamba, msimu mzuri wa kulima, nafasi kati ya mmea na mmea yaani formula ya upandaji, mbolea ya kutumia na mengineyo, asanteni.
 
Upo wapi mkuu..huku kwetu (shy)Njegere inalimwa mwezi wa 11 msimu wa mvua unapo anza na hua tayari kuvunwa mwezi wa kwanza..palizi ni mara mbili..
 
Naomba msaada kwa mwenye uelewa wa kilimo cha njegere
1. Yapi maeneo sahihi ya ulimaji
2. Upatikanaji wa maeneo husika na garama zake
3. Changamoto za kilimo hiki (faida na hasara)
4. Soko la njegere
5. Wapi au nani naweza mtembelea nikajifunza
6. Jarida, kitabu au blog yeyote ninayoweza pata taarifa sahihi
Na taarifa yeyote utakayoona inanifaa. Tafadhali ninaomba msaada wenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kilimo kina changamoto sana hasa kwenye bei unaweza kuta leo gunia elfu 50 afu kesho elfu 20!
Na kuna wakati zari linaweza kukudondokea unakuta unavuna Kila gunia laki moja!
Iringa ndo wanalima sana!

Soko ni kariakoo kama una mzigo mkubwa au unaweza amua kuwauzia wachuuzi ambao wanapeleka huko kariakoo!
Aina za mbegu ipo namba 3 na namba9
Hii namba9 mara nyingi inapandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua kwasababu haiwezi kuhimili mvua kubwa sana!
Ila namba tatu inaweza kuhimili mvua kubwa ndio maana hupandwa miezi ya January na kuendelea!

Ila unaweza panda kiangazi kwa kufanya umwagiliaji ila huwa changamoto ya dawa kwasababu hushambuliwa sana na ukungu, tofauti na ukipanda msimu wa masika huitaji kupiga dawa yoyote!!

Kwa kifupi ni ivo mkuu Ngoja wadau wengine waje wakupe nondo zaidi!
 
Nasi usisahau kutupa matokeo kwa kile utakachoambiwa,Ila njegere ni zao ambalo kulima na kuvuna kwake ni ndani ya kipindi kifupi sana,Wakati wa kuvuna ukaja bahatika ukakuta soko lipo vizuri basi wewe ni furaha hapo
 
Kama upo moshi tafuta shamba maeneo ya West kilimanjaro ndiko inakolimwa sana, wanunuzi kule wako wengi kutoka kenya wanafuata mzigo wenyewe shamba...
Asante mkuu, nilikua uko west kilimanjaro, sanya juu..nimejioneaa kwa kweli watu wanalimaa sana njegere, viazi, vitunguu... Nami pia ndio eneo iloilo ntalima njegere uzuri nilipata mwenyeji kule amenisaidiaa kwa kweli.
 
Back
Top Bottom