Msaada kuhusu kazi za machimbo Mererani

musicarlito

New Member
Dec 29, 2020
1
20
Habari wakuu,

Naomba mwenye taarifa au uzoefu na maeneo tajwa hapo juu kwa utafutaji

Kifupi nilibahatika kuajiriwa na taasisi kubwa ya kifedha hapa nchini, mshahara haukuwa mbaya, nilitaka kubadili mazingira ya kazi na kujiajiri kwenye biashara, vile isivyo bahati nilifeli.

Tangu hapo nilirudisha mpira kwa kipa(nyumbani), kusaidiana na familia kazi za kilimo, sijisifu ila niko hodari na mwenye bidii sana pia kwa kazi za mikono hasa kilimo, na lengo la kutaka kwenda huko ni kutafuta mtaji wa kilimo.

Kinachofanya kutaka kuachana nazo ni manyanyaso ya familia na kudharaulika hasa baada ya 'things to fall apart'...hii imefanya niamue kutafuta mwenyewe kwa njia yoyote ngumu halali, ilimradi heshima yangu iwepo.

Nitafurahi sana kwa michango yenu nyote hata ile ambayo sintoifurahia nitafurahi

Wenu katika kulijenga taifa

musicarlito
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom