Yagoole usijaribu ile inatafsiri word to word yaani neno katika sentensi linatafsiriwa peke yake. Hii itakusumbua kwasababu baadhi ya maneno hubadiri maana kutokana na matumizi.
Kweli tupu. Kulingana na dhana ya Uchavushaji katika nadharia ya Sarufi Geuzi Zalishi binadamu tuna uwezo wa kuibuka na sentensi mpya yo yote katika lugha yo yote tunayoimudu sawasawa. Watunga kamusi hawawezi kutabiri uchavushaji huu na wakijaribu basi wataishia kuandika likamusi likubwa kupindukia ambalo pengine halitakuwa na maana sana.
Katika kamusi nyingi, hata hivyo, wanachojaribu kufanya ni kutoa mfano tu wa sentensi chache ili kuonyesha muundo wa msingi wa lugha husika katika kiwango cha Sintaksia. Na hii mara nyingi hujikita katika salamu na sentensi zingine za muhimu kimatumizi.
Yagoole usijaribu ile inatafsiri word to word yaani neno katika sentensi linatafsiriwa peke yake. Hii itakusumbua kwasababu baadhi ya maneno hubadiri maana kutokana na matumizi.