Msaada kuhusu IPHONE 4S

Msaada kuhusu IPHONE 4S

Liobite

Senior Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
127
Reaction score
37
Habarini wanajamvi,
Naombeni msaada kuhusu simu yangu aina ya iphone 4s.Kila nikijaribu kuingia internet huwa inajizima na kujiwasha.Yaani toka nimekuwanayo sijawahi ku-access huduma ya internet.Kwahiyo naombeni ufumbuzi wa tatizo la simu yangu.
Nawasilisha!
 
Isije kua umeuziwa clone kama vipi icheki fresh napata shaka au weka specification zake hapa ili wadau wakija wawe na michango ya uhakika.
 
IPHONE 4S 64GB
Sio mtaalamu wa mambo haya ila kwenye box imeandikwa hivi;Supports UMTS HSDPA/HSUPA (850/900/1900/2100MHz) and GSM/EDGE (850/900/1800/1900MHz),Wi-Fi(802.11b/g/n),GPS,and Bluetooth 2.1+EDR.

Requirement;
Wireless service plan with AT&T required to activate all iphone features,Macor PC with USB 2.0 Mac OSXv 10.5.8 or later.
Window7,WindowVista or Windows XP Home or Proffesiondl (SP3).
ITunes9.2 or later required for some features (freedownload from www.itunes.com/download)
 
Igeuze nyuma halafu kwenye maandishi ya silver yaliyoandikwa iphone hapo chini yake kuna namba imeandikwa IMEI. Ikopi hiyo namba tuwekee hapa tukupatie majibu
 
Ebu jaribu kwenda kwenye setting then software upadate uone inasoma os ngapi na ujaribu kama unataka ku iupdate
kama itagoma kukupa ushirikiano basi itakuwa ni yutong.
 
IMEI baada ya kupiga *#06# imekuja hii;353056688607337
Na baada ya kwenda setting=>General==>About,kuna sehemu imeandikwa IMEI ambayo ni hii hapa:01296260524708
Na huku kwenye kava huku (nyuma ya simu) imeandikwa hivi IPHONE 4S (64GB)

Designed by Apple in California Assembled in America.
Model A1387 EMC 2430 FCCID:BCG-E2430A IC:579C-E2430A

MSAADA WENU NI MUHIMMU SANA KWANGU
 
Nimejaribu kwenda setting halafu kuna sehemu imeandikwa RESTORE ila nikijaribu kuweka PASSWORD inasema wrong pione password.

Sasa hapo sijui nifanyeje tena,NIMESHINDWA
 
IMEI baada ya kupiga *#06# imekuja hii;353056688607337
Na baada ya kwenda setting=>General==>About,kuna sehemu imeandikwa IMEI ambayo ni hii hapa:01296260524708
Na huku kwenye kava huku (nyuma ya simu) imeandikwa hivi IPHONE 4S (64GB)

Designed by Apple in California Assembled in America.
Model A1387 EMC 2430 FCCID:BCG-E2430A IC:579C-E2430A

MSAADA WENU NI MUHIMMU SANA KWANGU

Hahahahaha bro pole umeshikishwa kanyaboya
 
IMEI baada ya kupiga *#06# imekuja hii;353056688607337
Na baada ya kwenda setting=>General==>About,kuna sehemu imeandikwa IMEI ambayo ni hii hapa:01296260524708
Na huku kwenye kava huku (nyuma ya simu) imeandikwa hivi IPHONE 4S (64GB)

Designed by Apple in California Assembled in America.
Model A1387 EMC 2430 FCCID:BCG-E2430A IC:579C-E2430A

MSAADA WENU NI MUHIMMU SANA KWANGU
Hiyo obviously ni mchina aka CLONE!!,,,

Kuanzia original iPhone 4, 4S, 5, 5C na 5S zote haziandikwi capacity kwa nyuma. iPhone 2G, 3G na 3GS pekee ndio zenye capacity kwa nyuma.

iPhone Original zote zimeandikwa 'Designed by Apple in California, Assembled in China'!!! sio Assembled in America. Pole sana,,
 
Duuh,hapa nimeveshwa tayari.Ila nawashukuru wote kwa michango na mawazo yenu muliyoyatoa, maana mpaka sasa sina jinsi nimeibiwa tayari
 
Poleeee!

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
IMEI baada ya kupiga *#06# imekuja hii;353056688607337
Na baada ya kwenda setting=>General==>About,kuna sehemu imeandikwa IMEI ambayo ni hii hapa:01296260524708
Na huku kwenye kava huku (nyuma ya simu) imeandikwa hivi IPHONE 4S (64GB)

Designed by Apple in California Assembled in America.
Model A1387 EMC 2430 FCCID:BCG-E2430A IC:579C-E2430A

MSAADA WENU NI MUHIMMU SANA KWANGU

Kiongozi hapo bila kumung'unya maneno umeuziwa igizo aka "Clone" Products za apple za hivi karibuni hawaandiki size ya internal disc kwa nyuma na huwa hawaandiki assembled in America. Tatu iMEI namba ya kwenye Operating system na ya kwenye cover zinatofautiana. Pole sana japo ni sehemh ya maisha ya mwanadamu kujifunza kutikana na makosa
 
Back
Top Bottom