Msaada kuhusu hii BVM

Someni mchango huu kuhusu BVM kwa tahadhari sana. Ni program ambayo inataka ujiongeze (kwa lugha ya sasa hivi) na inahitaji masaa mengi zaidi ya kujisomea ukilinganisha na program nyingi za SUA. Ku-disco kupo asikudanganye mtu. Lakini ukiwa serious inawezekana. BVM wana probation tu na hakuna ku-carry forward kwa ujumla. Kila mwaka lazima ufaulu core courses ukianguka unaweza kuruhusiwa ku-retake (yaani huendi mbele bali utarudia lile somo na kulifanyia mtihani semester ambayo litafundishwa tena). Hapa ni mwaka mzima umesimama. Utakapofaulu ndio unakwenda mbele mwaka unaofuatia na utakuwa nyuma ya wenzako uliokuwa nao wakafaulu (first sitting au probation) kwa mwaka mmoja. Nia yangu si kutisha watu lakini afadhali ujue kile unachotarajia kukifanya kuliko kuambiwa kuwa BVM ni mteremko-ukweli ni mlima lakini watu hupanda na kufanikiwa.
 

Cc said duse
zingatia huu ushauri kwa umakini sana.
 
Daaah ahsanteni wakuu niko tayri kwa mazingira yeyte Yale kwa am ready to fight .
Napia naamini mungu yupo atanisaidia tuu kwan yey pekee ndio muweza na hakuna ajue mbele ila ni yeye tuu.
Hata nilikotoka nishawahi ambiwa unakoelekea kugumu zaidi so am going to cope with the situation.
Thanks a lot.
Niombeenj nichaguliwe.
 
Clear explanation!!!!!
 
sasa ni kozi gani chuo ni rahisi watu wengine bwana kozi yoyote ni ngumu na kila kozi watu wana disco urahisi au ugumu ni wewe mwenyewe ushauri wa hapa jamii forum hauwezi kukusaidia kitu ingia website ya sokoine university download prospectus angalia contents za kozi unayotaka kusoma ili uelewe unaenda kusoma nini kuliko kutegemea ushauri wa mtu kisa yeye ansoma hicho wanafunzi wa miaka hii wazembe sana kila kitu kinapatikana kwenye internet inasikitisha sana mtu anaenda chuo anategemea ushauri wa mtu eti hii kozi ikoje rahisi, ngumu halafu unajiita scientist.
 
Prospectus inasaidia lakini haikuambii kila kitu. Of course kuna swaga za vijana-lakini pia kuna ushauri ambao uko balanced. Ukisoma kwa umakini michango utapata ujumbe. Na pia sio wachangiaji wote ni wananfunzi ingawa michango ya wanafunzi ni muhimu kwani inakueleza kile kinachowakabiri.
 
Msisitizo tu.
Sie tuliaanza 105
Nasasa tupo 53.jiulize hapo wengine wameeenda wapi.kudisco,Ku retake ,kuacha mwenyewe tu kwa Ku salenda vyote vina wezekana kama hukuchukua tahadhari
 
Neurosurgeon
 
Kwenyw Prospectus hupati kila kitu.
Ukweli ni kozi ambayo utakua Bize sana kuliko kozi zote pale SUA.

Siasa za vyuo huwezi shiriki na sometimes migomo inayotokea mavyuoni, ukiwa unasomea kozi hii huwezi thubutu kushiriki migomo.
Wenzenu wakiwa wamegoma, profu amaweza ingia darasani akaendeleza lecturing.
Ni kozi ambayo haiko huru kama zingine.

Sikukuu za kitaifa na likizo mbalimbali itabidi uzisahau, yaani uwaachie watoto na wadogo zako nyumbani.

Mazingira haya na sababu nyinginezo huwafanya watu kutotamani ku- opt kozi hii.
So ukisikia BvM, utambue hii ni special case pale SUA.
 

Haaaaaaaaaaaaa mkuu vice versa is true!!!njoo tunaanza na screen test
 
Msisitizo tu.
Sie tuliaanza 105
Nasasa tupo 53.jiulize hapo wengine wameeenda wapi.kudisco,Ku retake ,kuacha mwenyewe tu kwa Ku salenda vyote vina wezekana kama hukuchukua tahadhari
Mkuu nadhaniii tupo class 1 .... Yaanii originalll nadhaniii tumebaki 45 maaNa hao wengine tumewakuta njianiii
 
Mkuu nadhaniii tupo class 1 .... Yaanii originalll nadhaniii tumebaki 45 maaNa hao wengine tumewakuta njianiii
Sikudhania kuwa hali ni mbaya kiasi hiki!!!!!!!! Mtafanikiwa tu.
 
Kaka ugumu wake unaweza kuwa kama advance ukisoma PCB/pcm au huko pagumu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…