habar zenu wana jf. mie sio mzofu sana katika hili jikwaa. nimekua nikiona post za wenzangu zikiwa na nakshi za aina mbali mbali tofauti na post zangu. kwa hiyo ningependa kujua
2. Codes zinazotumika ku andika username ya mwana jf kwenye post na lile jina linakua linautofaut na maandish mengine..
3. Codes za kuweka alama mbali mbali kama zinazoashiria kicheko, mshangao n.k kwa mfano mie najua moja hii apa :typing: ambayo unaiweka kwa kuandika :typing/: bila slash.
Zipo coding methods nyingi sana na kama una uzoefu na html coding basi itakuwia urahisi.
[mention]=kama unataka kutaja jina la mtu na jina hilo huwekwa kati ya parandesi
[quote=xxx][/quote]=kama unataka kuweka nukuu, hizo xxx huwakilisha jina la mtu unayemnukuu kama ni nukuu toka kwa huyo mtu
[url=xxx]AAA[/url] = kuweka kiunganishi kiwe cha ndani ya JF au nje, katikati ya hizo parandesi palipo na AAA unaweka maandishi ambayo unataka yawakilishe kiunganishi chako. xxx ni full url address ambayo inabeba nukuu utakayo kuiweka
[img][/img] = Hii ni kwa ajili ya kuweka url yenye kuwakilisha picha utakayokuijumuisha na url hiyo inakaa katikati ya parandesi
[h][/h] = Hii ni kwa ajili ya msisitizo wa Heading
[center][/center] = Kuweka maandishi au picha katikati, ukitaka yawe KULIA au KUSHOTO basi huna budi mahali pa CENTER ukatumia maneno RIGHT au LEFT
[color=xxx][/color] = Kuweka rangi maandishi yaliyopo katikati ya parandesi, xxx huwakilisha jina la rangi au color code..
[b][/b] = Kuyafanya maandishi yaliyopo katikati ya parandesi yawe bolded