Msaada kuhusu chanjo ya Homa ya Ini

Msaada kuhusu chanjo ya Homa ya Ini

kakamgeni

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2018
Posts
241
Reaction score
201
Asalaaam Aleikum Great Thinkers,

Ningependa Niwatakie Heri Ya Mwaka Mpya Wa 2020, Najua Wapo Wengi Walitamani Kuuona Lakini Haikuweza Kuwa Bahati Kwao, Sio Kwamba Sisi Ni Wakamilifu Sana Au Wema Ila Ni Kwa rehema Zake Mwenyezi Mungu.

Wahenga Wanasema Kwenye Wengi Kuna Mengi. Nikienda Moja Kwa Moja Katika Dhumuni Thread Hii, Ni Kuhitaji Ufafanuzi Japo Kwa Ufupi Kuhusiana Na Hii Chanjo Inayotangazwa Na Serikali "CHANJO YA HOMA YA INI" Nimekuwa Nikifuatilia Matangazo Na Baadhi Ya Mijadala Sehemu Mbalimbali.

Wapo Watu Kwa Mujibu Wao Wanadai Kwamba Ukipata Chanjo Ya Ini Kinachotokea Katika Mwili Inakuwa Ni Kama Vile Umeliweka Ini Kwenye Mfuko Wa Plastic, Hivyo Huenda Kwa Baadae Ikaja Kuleta Tatizo kubwa Zaidi.

Hivyo Ningependa Kupata Ufafanuzi Kwa Wale Wenye Uelewa Kuhusu Suala Hili. Wazee Wa Matusi, Kuwahi Siti Na Kejeli Pia Mnakaribishwa Maana Kwenye Msafara Wa Mamba Kenge Pia Wapo.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo habari za mfuko wa plastic ni mbwembwe za kufikisha ujumbe,wewe elewa ya kwamba unavyopewa chanjo, hiyo chajo inasababisha/inachochea mwili kutengeneza kinga (antibodies) zenye uwezo wa kuzuia maambukizi ya kirusi anayesababisha homa ya ini (hepatitis b).
 
Mm sio mtaalamu wa afya lakn sidhani kama kuna ukweli wa ulichokisema juu ya chanjo!!
Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa chanjo ni bacteria/virus waliopoozwa na hivyo hawana madhara yeyote mwilini!! Lengo ni kustimulate mfumo wa ulinzi mwili hivyo mwili huzalisha askari wengi kwa ajili ya kupambana na bacteria/virus wa aina ile!! Hivyo mwili hupata ulinzi ndio maana hawawezi kuugua aina ya ugonjwa ule
 
Hivi hawa wanaogundua chanjo kwa nini wasifanye kutafuta chanjo ya HIV?
 
Ni ngumu sana kupata chanjo ya HIV sababu HIV anabadilika kila siku(Mutation) na pia kuna strain tofauti za HIV virus.
Yani ukitengeneza chanjob ya HIV mwaka huu baada ya muda haifanyi kazi kabisa maana ni kama virus anabadilika na amekuwa mwingine.
Hivi hawa wanaogundua chanjo kwa nini wasifanye kutafuta chanjo ya HIV?
 
Nilipata Hepatitis B mwaka 1978 nilipewa miwa na maji mengi ila kuna daktari alinichoma sindano karibu iniue. Nilipona.

Mwaka 1994 nilipewa kinga ya H. a and c dose tatu na nikamaliza. Kuanzia pale kila nikienda medical Examinationa Annual huwa naambiwa nina kinga ya H ab and c. Ninaamini ukipata kinga au ukishaugua unakuwa umejijengea kinga sababu hizi ni virus siyo bacteria infection kusema zinajirudia.

Yes unaweza kupata magonjwa ya ini kama Fat liver lakini siyo hizo zingine. Naomba kukosolewa maana mie siyo dakatri ila nafanya checkup ya mwili wangu kila mwaka. Nimeambiwa nina mafuta kidogo kwenye ini hivyo nipunguze unene. Nimepunguza kilo 7 za unene wangu na najisikia vizuri.
 
Nilipata Hepatitis B mwaka 1978 nilipewa miwa na maji mengi ila kuna daktari alinichoma sindano karibu iniue. Nilipona.

Mwaka 1994 nilipewa kinga ya H. a and c dose tatu na nikamaliza. Kuanzia pale kila nikienda medical Examinationa Annual huwa naambiwa nina kinga ya H ab and c. Ninaamini ukipata kinga au ukishaugua unakuwa umejijengea kinga sababu hizi ni virus siyo bacteria infection kusema zinajirudia. Yes unaweza kupata magonjwa ya ini kama Fat liver lakini siyo hizo zingine. Naomba kukosolewa maana mie siyo dakatri ila nafanya checkup ya mwili wangu kila mwaka. Nimeambiwa nina mafuta kidogo kwenye ini hivyo nipunguze unene. Nimepunguza kilo 7 za unene wangu na najisikia vizuri.
Kwahiyo Unanishauri Nichome Sio Mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm sio mtaalamu wa afya lakn sidhani kama kuna ukweli wa ulichokisema juu ya chanjo!!
Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa chanjo ni bacteria/virus waliopoozwa na hivyo hawana madhara yeyote mwilini!! Lengo ni kustimulate mfumo wa ulinzi mwili hivyo mwili huzalisha askari wengi kwa ajili ya kupambana na bacteria/virus wa aina ile!! Hivyo mwili hupata ulinzi ndio maana hawawezi kuugua aina ya ugonjwa ule
Asante Mkuu Kwa Ushauri Wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom