Msaada kuhusu calendar ya wanawake

Msaada kuhusu calendar ya wanawake

Wakuu amjambo

Ningependa kujua nikwamba kila mwanamke hutembelea calendar hii ya siku za hatari inayoanzia kwenye tarehe 11 adi tareh 18 ? Au kila mwanamke Ana yakwake maana nais kuna manzi anataka kutegesha bomu .
Habari,
Msingi wa kutumia kalenda ni pale ambapo utafahamu kama mzunguko wa mwanamke/ aliyeko kwenye umri wa kupata watoto na yuko sawa mhusika ni:

A: MFUMI WA UTOKAJI WA DAMU/HEDHI KWA MWEZI
1: Regular (hujirudia kwa kiasi kilekile).
2: Irregular (mzunguko hubadilika idadi ya siku kila mara).

Maelezo yanayofuata yanamhusu yule wa namba moja/regular. Wale wa namba mbili wana utaratibu tofauti kuwafuatilia.

B: UREFU WA MZUNGUKO
Urefu wa mzunguko hutofautiana kutoka mwanamke mmoja mpaka mwingine lakini wote walioko sawa, mzunguko wao ni kuanzia siku 21 mpaka siku 35.

1: Siku 21-25 mzunguko mfupi
2: Siku za mzunguko wa wastani 26-32
3: Siku 33-35 mzunguko mrefu

C: KUANDAA YAI NA MJI WA MIMBA
1: Siku za kuandaa yai mpaka kupevuka ni hutofautia kwa kila mwanamke kulingana na urefu wa mzunguko, hivyo siku za kuandaa yai zaweza kuwa siku(7-21)kwa akina mama wote kulingana na urefu wa mzunguko yaani mfupi mpaka mrefu. Kama ilivyoelezwa kule juu.

2: Siku kutoka yai kukomaa/ovulation mpaka damu kutoka/hedhi ziko sawa kwa kila mwanamke yaani ni siku 14 kwa wanawake wote.

Kwa msingi huo, ili kujua mwanamke alitoa yai/hutoa yai lini: chukua urefu wa mzunguko wake toa siku 14, yaani idadi ya jumla ya siku zilizopo kutoka siku ya kwanza ya mzunguko mmoja/ kuona hedhi mpaka siku ya kwanza ya hedhi ya mzunguko unaofuata/kwa wale wenye mizunguko sawa tu.

D: SIKU YA KUTOA YAI VS SIKU YA DAMU KUTOKA
Siku ambayo yai hukomaa/hutoka, ndiyo siku ambayo yai huweza kukutana na mbegu ya kiume na kutengeneza mtoto(fertilization).

Yai likishatolewa huduma katika uhai wake kwa saa 24 tu. Baada ya hapo yai huwa kwenye hali isiyoweza kutunga mimba (loss of fertility).

Kutoka kupoteza uwezo wa yai kutunga mimba mpaka unapoona damu ya hedhi ni siku 14. Katika kipindi hiki chote mimba haiwezi kutungwa. Siku hiyo ya 14 mji wa mimba humpukutika kwa ule ukuta ulioandaliwa na hapo ndo damu hutoka.

Hivyo, ili kujua lini upate mtoto au ukwepe kupata mtoto ni vyema kuitafuta siku ya yai kutoka/ovulation. Kulingana na sifa la yai kuishi saa 24 baada ya kutolewa na mbegu za kiume kuishi saa 48, hii ndo huleta ongezeko au punguzo la siku tatu ili kukwepa kulikuta yai likiwa hai au mbegu kulisubiri yai.

Mfano:
1: Mzunguko wa siku mfupi:
Siku 21 toa 14=siku 7 kwa mzunguko mfupi/yai kupevuka/ovulation.

Jumlisha au kutoa siku tatu7+3=siku ya 10 Vs 7-3= siku ya 4.

Epuka au tumia siku ya 4 mpaka 10 kulingana na lengo.

2: Mzunguko wa kati:
Mzunguko wa siku 28-14= siku14 yai kupevuka/ovulation.

Siku 14+3=siku17 na 14-3= siku11

Epuka au tumia siku ya 11 mpaka 17 kulingana na lengo.

3: Mzunguko mrefu:
Siku 35-14= siku 21
Siku 21+3=siku24 vs siju 21-3=siku18
Epuka au tumia siku ya 18 mpaka 24 kulingana na lengo.

NB: Zingatia pia mzunguko wa mwanamke huweza kubadilika kutokana na stress, kazi nzito na mabadiliko ya hali ya hewa kama kusafiri toka mkoa mmoja mpaka mwingine nk.
 
Back
Top Bottom