Kimtandao, utahitajika uwe na Website unayohitaji na itakuwa kubwa kulingana na watu wanaopost bidhaa. Ukumbuke bidhaa itawekwa na watu tofauti tofauti kwa categories tofauti hivyo itahiji moderators na maintainers wa hiyo site(Kwa site ndogo siyo tatizo wanaweza fanya wawili au mmoja) ila watu wanavyokuwa wengi na uvunjaji wa taratibu unakuwa mkubwa utahitaji moderators wengi pia.
Kwenye utengenezaji hakuna tatizo ukishatengenezewa site utapewa maelezo ya wewe kama admin namna ya kuitumia. Na kwa site kubwa kama hii ya E-Commerce kuwa na IT guy ni muhimu. Nyakati nyingine siyo kila kitu kitakuwa automated kuna muda itahitaji manual configuration.
Unaweza kupata pesa unapokuwa na wauzaji wengi, unaweza kuwacharge wauzaji walipie kiasi fulani cha pesa ili matangazo yao yawe ya kwanza(juu) muda wote ili kuonwa na wanunuzi wengi. Unaweza pia kuwa na shipping company yako bidhaa zote zinazonunuliwa kwenye website yako uwe unazifanyia shipping wewe na unaingiza hiyo shipping cost. Unaweza pia kucharge percent fulani kwa muuzaji kwa kila bidhaa atakayofanikisha kuuza. Na mengine, na mengine...
Kubadili host inawezekana mkuu.