Nilichukua ile business kadi yake huku mawazo yakinipeleka mara ya mwisho nilipomuona huyu dada, nakumbuka alihama shule ghafla tukapotezana. Kipindi kile sababu ya ujana wangu nakumbuka nilishawahi kutoka nae siku moja baada ya party na vinywaji. Ingawa baada ya hapo sikuendelea na urafiki nae wa karibu na nilikuwa ninamuepuka, mpaka alipohama. Baada ya kuweka ile kadi mfukoni ninapiga jicho kiti cha nyuma... Mungu wangu!!!???, Kidogo nianguke kwa kizunguzungu..... ni kama nilikuwa natazama kwenye kioo, yaani mtoto kadri ya miaka saba ananifanana utafikiri ninatazama picha yangu....