Msaada: Kuacha kadi ya Gari wakati wa kukopa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Kuacha kadi ya Gari wakati wa kukopa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by tovuti, Oct 9, 2012.

 1. tovuti

  tovuti Senior Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau nilikuwa nataka kukopa milioni 3..., namwachia gari akae nayo mpaka nitakomlipa kwa miezi 2 na rate ya 20%

  Sasa huyu jamaa kaniambia nikimwachia gari niwache na kadi yake original, na akaniambia kuwa watu wote

  wanaokopesha wanafanya hivyo....

  Wadau nilikuwa nauliza kuwa ni sawa? na hapo nitakuwa safe side nikiwacha kadi original ya gari?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kwa nini ukakope mtaani? Yaani umwachie kadi na gari?
  Huko mtaani unamwamini kiasi gani?
  Kwa nini usikope benki na gari liwe collateral?
  Huko benki utawaachia tu kadi original na itatunzwa salama kwenye safe za strongroom zao.....
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  Jambo hilo litakugharimu sana.
  Siku moja nilikuwa kwenye Gari, na pembeni yangu walikuwapo kin mama wawili na mazungumzo yao yalikuwa hivi "KUNA WATU WANATUMIA NGUVU ZA GIZA/KICHAWI ILI KUPATA MALI ZA WATU. WAMEANZISHA/WANATOA MIKOPO LAKINI WATU WATU WANAO KOPA LAZIMA WAWEKEZE GARI/NYUMBA AU SHAMBA. SASA KUNA MTU MMOJA ALIKOPA 5,000,000/= KWA MASHARTI YA KUWEKEZA MAGARI 3.NA ALITAKIWA ALIPE BAADA YA MIEZI MITATU, LA SIVYO MAGARI YAKE YATACHUKULIWA. yULE MTU KWA KUWA ALIKUWA NA UHAKIKA WA KUPATA PESA ZA KULIPA, ALIKUBALI. BAADA TU YA KUCHUKA ZILE PESA, YULE ALIYEMKOPESHA AKAMUULIZA JE, NI KWELI UTAWEZA KULIPA? JAMAA AKAJIBU NI KWELI NITALIPA.

  BAADA YAHAPO, NJIA ZOTE ZA KUPATA KIPATO ZA YULE ALIYE KOPA ZILIFUNGA, NA ALIPOONA ZIMEBAKI SI CHACHE MKATABA HUISHE, ALIONA NI BORA AUZE GARI MOJA KATI YA YALE MATATU ILI ALIPE DENI. SHIDA IKATOKEA KUWA WATEJA WA KUNUNUA GARI HAWAPATIKANI. ILIBAKI WIKI MOJA YA MKATABA, NDIPO AKAENDA KWENYE MAOMBI NA KUELEZA KISA KIZIMA, ALIFANYIWA MAOMBI NA ALIPATA MTEJA WA KUNUA GARI LILE KWA 5,000,000, NA ALIPOMPELEKE MDAI WAKE, AKASHANGAA SANA NA KUMWAMBIA "HAMA KWELI UMEWEZA KULIPAJE, SIKUTEGEMEA KABISA KUWA UTAWEZA KULIPA. KWELI WEWE NI BINGWA NA UMENIWZA.

  KUNA WATU WENGI WAMEPOTEZA NYUMBA/MASHAMBA NA VITU VINGINE KWA NJIA HII. KUWA MAKINI.
   
 4. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  mkuu apo juu ushauri wako utasaidia watu wengi
   
 5. tovuti

  tovuti Senior Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asanteni kwa waliochangia.... Wengine karibuni kutoa mchango wenu
   
 6. tovuti

  tovuti Senior Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nataka mkopo wa muda mfupi.....Benki nimeambiwa wanatoa mkopo wa muda mrefu, na nafikiri pia watakuwa na process ndefu
   
 7. Kig

  Kig JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 1,060
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kaa ufikirie mara mbili mbili kabla ya kukubali masharti ya namna hii kwenye mikopo. Watu wengi wanadhulumiwa sana bongo hata sababu ya msingi. Wakopeshaji wengi ni wakorofi sana maana wanatafuta faida kwa kila mbinu. Ukiweka dhamana ya kitu chenye dhamani kuliko hela uliyokopa atakuwa anakuombea ushindwe kulipa. Mfano kama unakopa milion 3 halafu unamwachia gari yenye dhamani ya million 6 au zaidi, lazima atafurahi ushindwe kulipa deni ili afaidi gari maana atauza kwa faida kubwa. Uwe makini sana.
   
 8. tovuti

  tovuti Senior Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa ushauri.....lakini sina jinsi lazima nikope
   
 9. Lait noir

  Lait noir Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sasa mkuu ulitakaje kwani? Ukopoe alafu umuachie gari bila Kadi? Kadi ndio gari bana, kama umedhamiria kukopa na kuweka gari rehani ni lazima uache kadi
   
 10. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkuu hii mimi imewai nitokea kabisa, yani siku nampigia jamaa simu nimpelekee fedha yake, akupokea simu kilichofuata ni msg tu, kwamba zimebaki siku mbili na gari keshapata mteja siku ya kurejesha kama sitapeleka pesa basi anauza, hakuna kuongezewa muda wala nini, kwakuwa watu walikuwa wameshaniambia kwamba jamaa anajiamini wala sikujisumbua kumpigia, siku iliyofuata asubuhi nimedamkia kwake, jamaa anatoka ananikuta mimi nimeshika kijibaasha kangu na namwambia nataka kadi na funguo ya gari yangu, aliniuliza mara kumi kumi nimewezaje kumlipa, baadae ndiyo nikaja sikia kwamba jamaa anatumia nguvu za giza kuwedhulumu waliokopa kwake.

   
 11. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  rejea kisa cha mfanyabiashara (RIP) aliyeweka hati ya nyumba yenye thamani ya 600m kwa papaa musofe ili akopeshwe 30m later on papaa akamchezea deal na kutengeneza hati zinazoonesha aliinunua ile nyumba, mfanyabiashara amerudisha 30m apewe hati papaa hazitaki, mfanyabiashara kakimbilia mahakamani (2010) kudai haki yake, wakati kesi bado ipo mahakamani mfanyabiashara akapigwa risasi ya kichwa na watu wasiojulikana, papaa ametoa ile hati ya nyumba anayodai aliinunua kwa marehemu na kumtaka mjane aondoke haraka kwenye lile jumba na alifanikiwa kumtimua kwa mabavu kama ulivyoona kwenye TV mwaka jana... kwasasa papaa yupo lupango kwa tuhuma za kupanga mauaji
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  haraka haraka inaponza.....

  Benki wala hawachukui muda mradi waverify tra kuwa gari ni lako....

  Na muda si tatizo unaweza kuchukua mkopo ukasema utalipa ndani ya miezi 6 lakini ukipata hela ndani ya hiyo miezi miwili unaenda unalipa nz deni unafuta, tena unaweza kuprwa hata mkopo mkubwa zaidi
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mikopo ya aina hii wengi huishia kuibiwa....
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mwache akitafute kiranga chake......
   
 15. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Nenda benki ndugu, haraka haraka itakutokea puani. Nenda hata benki ya posta wako fasta achana na hao wazushi wa mtaani!
   
 16. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kaka kuwa makini watu wengi wamepoteza magari na nyumba zao kwa ajili ya mikopo aina hiyo kama huamini naomba uende masai camp baba ilala kuna jamaa amefunguwa yadi kubwa ya kuuza magri ya watu anaowakopesha wote wanapoteza magari yao huyo jamaa anaitwa doni na mpare no. Simu yao 0716834333 ukikopa tu ujuwe hilo gari limeondoka sio lako tena , ni sawa umemuuzia kwa bei ya kutupa
   
 17. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Dah, JF ni elimu tosha
   
 18. C

  Changamoto2015 JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  nenda kajaribu equity bank kama upo dar es salaam
   
 19. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Wanabodi, kweli JF ni GT. Ni Chuo Kikuu. VIVA JF.
   
 20. d

  demulikuy JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 80
  Dont do that. Hizo arrangements are stacked against you, kwa sababu probability ya kwamba utarudisha in time with 20% interest ni kidogo sana, hence the probability of losing ur car is high. Mkataba ho umelenga kulipata gari lako kwa bei chee basi full stop. Style hii imeenea sana nchini has Dar. Kwa kiasi hicho cha mkopo, nenda kakope Bank au SACCOS kama wewe ni mwanachama.
   
Loading...