Msaada: Kompyuta yangu haiwaki

talimbo

Member
May 9, 2013
8
2
Nina pc (desktop) dell duo core nilikuwa naitumia hom ghafla ikazima kila nikiiwasha taa tu ya kwenye button ya kuwashia inawaka kama indicator ya gar lkn haizungushi fan wala machine haiboot cjui tatizo ni nn msaada wenu pliz.
 
Pole saana mkuu, huo ndio ujinga wa dell, kiuhakika diode za moto zishakunya. Bahat mbaya kufix hilo tatizo ni mtihani mkubwa sana, jamaa zangu washatupa desks zao karibia 4 ,

Peleka kwa technician ila kama ni suala la diode, kupona ni 20% .

Kwa ushauri. Ukinunua mashine nunua HP wapo vizur sana maeneo yenye power interuptions
 
dah yani mkuu hiyo ni kama yangu h
aijawaka hadi leo.
but nilijaribu kuingia youtube wakasema nichomoa power cable nihold power botton kwa sekunde kama kumi hivi. alafu nichomeke tena power cable kisha niwashe. nikafanya hivo lakini haikuwaka hadi leo.

ipo tu nataka ninue nyingine nichukue tu baadhi ya hardware kama gpu, ram,hdd na dvd writer.
 
Nina pc (desktop) dell duo core nilikuwa naitumia hom ghafla ikazima kila nikiiwasha taa tu ya kwenye button ya kuwashia inawaka kama indicator ya gar lkn haizungushi fan wala machine haiboot cjui tatizo ni nn msaada wenu pliz.
je haitoi alarm yoyote?? kama inawasha taa kwa ku-blink na kukata tatizo litakua ni capacitors,transistors au power supply na repair yake inawezekana kabisa..
 
Sikia Bro
Fungua PC Yako Hapo Afu Chomoa RAM Zote chukua kitambaa Kizuri Zifute Katika Meno yake Kisha Weka RAM Moja Moja Kwama Zipo Nyingi Na Uwashe I Hope Mashine Itawaka.
Pia Isipowaka Toa Betri ya saa Inayokuwemo Acha Kwa dakika Tano Kisha Rudia Tena Zoezi la Kwanza.
PC za DELL sio Mbovu kama Wanavyosema Ila Iko Hivi
Dell ndio kampuni ya kwanza kueneza sana pc zake na kuziuza sana na pc nyingi walizokuwa wanatumia watu ni ID ambazo zipo katika mfumo wakizamani na hizi ndio pc ambazo zinasumbua sana na si kampuni ya dell tu ni pc yoyote tu ili mradi ikiwa ID.
inaweza kuwa nzima na ikazima tu pasipo sababu inahitaji mtu mzoefu nazo sana kuweza kuzihandle hata fundi asipojua tabia ya hizi mashine basi inakuwa ni kasheshe sana kuweza kusolve maana anakuwa anabahatisha.

Ila Kwa Ulimwengu Huu Mashine Zote Zimebadirika Zinakuwa Ni Mashine Za Mfumo Wa SATA ambazo ni Imara sana hakuna mfano.
na hakuna PC zinazovumilia mikiki mikiki kama PC za kampuni ya DELL Muhimu ni wewe ujue hii ni SATA au ID ikiwa SATA hizo ndio mashine mpya zinapiga kazi mpaka unaweza ogopa kwahiyo DELL sio mbovu kama wanavyosema.
Na DELL ndio kampuni pekee ya PC ambayo INauwezo waKuwaka Siku SAba Bila kuzima na inapiga kazi na haipati MOto
Nunua Mashine AMbayo Ni SATA baasi mwisho wa matatizo,
ingia makampuni kibao utakutana na DELL kaka fanya Uchunguzi wako utaniamini kaka.
 
Kwa NJia Nilizokupa Isipowaka We NJoo PM Naamini Itawaka TU Hilo Sio tatizo La Pc Kufa Kama Inawasha Taa kama indicator.
na Sio tatizo Kubwa Hilo
 
Hili ndio suluhisho sahihi kwa PC yenye tatizo Kama hilo. FUNGUA PC YAKO KISHA NENDA PALE KWENYE PROCESSOR FUNGUA ILE COOLER UTAONA PROCESSOR ANGALIA KAMA NI PIN AU PINLESS ITOE ZAFISHA SEHEMU INAPOKAA KWA PETROL THEN IRUDISHE KISHA PAKA HEAT SINK IKIGOMA TAFUTA HICHO KI PROCESSOR KINGINE. NIMEWAHI MALIZA HILO TATIZO KWA NJIA HIZO MARA KADHAA.
 
je haitoi alarm yoyote?? kama inawasha taa kwa ku-blink na kukata tatizo litakua ni capacitors,transistors au power supply na repair yake inawezekana kabisa..
Mkuu mimi nina tatizo kama hilo pc yangu aina ya hp desktop nilikuwa naitumia vizuri tuu nikamaliza shuhuli yangu kwenye kompyuta yangu na nikaizima vizuri tuu nikawa nimekaa kama masaa mawili nikataka niitumie tena basi ile nawasha tena inawaka taa nyekundu ambayo sijawahi iona ikiwaka tena inawaka kwa ku-blink na inapiga alarm kiukweli mimi ni mgeni kwa maswala hayo hiyo naomba mnisaidie tafadhali nipate kujua je hili ni tatizo kubwa?na linatatuliwa vipi? Ila yangu feni inazunguka mkuu
 
Sasa hapo computer inakuambia tatizo we sikiliza beep ni ngapi na sequence ipo vipi? Mfano inaweza beep nyekundu Mara 4 Kisha inaacha inabeep tena Mara 4 kichwa inaacha.
 
Yangu ina tatizo kama hilo inapiga alarm na feni linazunguka
Chomoa umeme ,Chomoa RAM zote kam zipo zaid ya moja toa cmos batt safisha RAM slot (sehemu zinapo kaa Ram ) hold power button for at least 20sec then rudishia kila kitu yaan RAM na cmos batt washa pc
 
Sasa hapo computer inakuambia tatizo we sikiliza beep ni ngapi na sequence ipo vipi? Mfano inaweza beep nyekundu Mara 4 Kisha inaacha inabeep tena Mara 4 kichwa inaacha.
Boss hujanimaliza kunieleza kaka maana inawaka taa nyekundu badala ya njano na inapiga alarm nakuomba uendelee kunisaidia tafadhali
 
Boss hujanimaliza kunieleza kaka maana inawaka taa nyekundu badala ya njano na inapiga alarm nakuomba uendelee kunisaidia tafadhali
Beep zipo ngapi zisikilize na taa zipo ngapi zinawaka kwa muendelezo upi? Ni rahisi kujua tatizo lakini mpaka maelezo yako yakae sawa.

Kama huelewi chukua video post humu.
 
Kwa NJia Nilizokupa Isipowaka We NJoo PM Naamini Itawaka TU Hilo Sio tatizo La Pc Kufa Kama Inawasha Taa kama indicator.
na Sio tatizo Kubwa Hilo
Ni kweli kabisa, maadam inawasha taa maana yake hata mother board ni nzima , hapo kuna kitu kidogo tu kimetumba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom