Msaada; Kifaa gani hiki?

ni kifaa cha kupimia pombe ya Moutai(aina ya pombe ambayo ni maarufu sana nchini China) ili kuikagua kama ni pombe ya kweli au bandia.
Asante Bakari kwa kuitikia wito,vipi hio pombe ina gharimu kiasi gani?
 
Asante Bakari kwa kuitikia wito,vipi hio pombe ina gharimu kiasi gani?
bei yake hutegemea muda wa kuanzia ilipotengenezwa. Pombe hii yenye umri zaidi ya miaka 50 itachukua RMB20000(TSH milioni 7.16). hata yenye umri wa miaka 3 huchukua zaidi ya RMB1000(TSH laki 3)
 
sawa mkuu tutawasiliana PM huko nitakutafuta
sawa unakaribishwa wakati wowote.
sasa ni saa 5:18 hapa. kesho tutafanya mtihani wa mwisho unaohusu fasihi ya kiswahili, kwa hivyo nahitaji kulala mapema, naomba msamaha wako sitaweza kuzungumza nawe kwa muda mrefu sana. Jumatano baada ya mitihani yote kumaliza nitakuwasilisha ujumbe kwa PM au hata kwa Wechat.
 

sawa mkuu hakuna Tatizo nitumie ujumbe siku ya jumatano PM
 
bei yake hutegemea muda wa kuanzia ilipotengenezwa. Pombe hii yenye umri zaidi ya miaka 50 itachukua RMB20000(TSH milioni 7.16). hata yenye umri wa miaka 3 huchukua zaidi ya RMB1000(TSH laki 3)
Aisee,bei ghali sana
 
Jaribu kufanya google search kwa picture na kuhusu maelekezo tumia google translater kupata translation kwa pic catcher
 
Mhe. Mwalimu Nyerere aliwahi kuzuru China mara kadhaa. Kila alipofika, waziri mkuu wetu Zhou Enlai alikuwa humzawadia pombe hii. Ilipendezwa sana na Mwalimu Nyerere.
Aisee safi sana,kumbe Baba wetu wa Taifa alikua anapenda MAOTAI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…