Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
(Baadhi ya maelezo ni kutoka katika kitabu cha John Gray kinachoitwa 'Men are from Mars, Women are from Venus' Chapter 8, ukurasa nambari 87)
Hisia ndio msingi mzito katika mahusiano ya mwanamke na mwanaume, hapa sielezei haya mahusiano ya bei rahisi ya ku date kisa tu mmeamua ku date, hapa naelezea mahusiano ya kweli ya wale waliopendana, wenye hisia za dhati na malengo yao binafsi.
Ukweli ni kwamba kila kiumbe yaani mwanamke na mwanaume, kina mahitaji yao binafsi ya kihisia tofauti na mwenzake. Suala la mahusiano kuvunjika linakuja pale ambapo watu huingia kwenye mahusiano bila kujali, kutambua, kuheshimu au kuthamini mahitaji ya mwengine.
John Gray, anasema kwamba "kwa upande wa wanawake Mawasiliano ndio nguzo kuu ya hisia zao. Hawa viumbe wanahitaji sana kusikilizwa na kupewa nafasi ya kujaliwa. Ni lazima ujifunze kusikiliza hisia za mwanamke, utamvutia mwanamke ikiwa tu utajali, utaelewa, utaheshimu, utathamini, utazingatia na kutilia maanani hisia zake"
Sio mada ya upumbavu, lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi wanafeli pale ambapo wao huchukua maamuzi yale ambayo mwanamke kaamua kuchukua. Mfano: Ukitokea mgogoro au hali ya kutokuwa na furaha pale ambapo mwanamke anakaa kimya basi mwanaume na yeye anaamua na yeye kukaa kimya eidha kumkomoa mwenzi wake, au kujaribu kutaka kuona nani atakuwa wa kwanza kumtafuta mwenzake au kujaribu kuonesha kuwa hata yeye hajali 'lolote na liwe'. Hii kitu inaua sana mahusiano, kama mwanaume unaejielewa huwezi kukubali kushindana na mwanamke kamwe.
Kitabu cha Men are from Mars, Women are from Venus kimejikita kwenye nadharia kwamba 'wanawake kwenye mahusiano wanaonyesha hisia ambazo wao wenyewe wanataka kuonyeshwa, na wanaume wanaonyesha hisia ambazo wao wenyewe wanataka kuonyeshwa. Hapo ndipo kutoelewana kunatokea, ilitakiwa mwanamke aonyeshe hisia ambazo Mwanaume anazitaka na mwanaume aonyeshe hisia ambazo mwanamke anazitaka. Yaani shida ipo pale ambapo kila mtu anatoa kile ambacho anataka apewe, badala ya kutoa kile ambacho mwenzake anakitaka.'
Pole na nisamehe sana kama hujanielewa, ila unaweza kuchukua maamuzi ya kusoma kitabu cha Men are from Mars, Women are from Venus ili uelewe zaidi kwa muda wako.
Ahsante kwa kunisikiliza, ni mimi [emoji2398] Amani Dimile
#amanidimile #misemo_ya_hekima #tungomaridadi #fikrazadimile #malengamtoto #menarefrommars #womenarefromvenus #menarefrommarswomenarefromvenus