Msaada katika MAZOEZI.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada katika MAZOEZI....

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtalingolo, Dec 23, 2011.

 1. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Katika sector ya Afya mbali na kula vizuri, tunashauriwa pia kuipa mazoezi miili yetu.
  Sasa wadau ningependa kuuliza je ni mazoezi gani inashauriwa tufanye, wakati gani na faida zake ktk miili yetu (for both male and female)??

  Nawasilisha.....
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO

  Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.

  Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.

  Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.

  Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
  Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi,

  kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …

  Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.

  Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.

  UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI

  Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya

  mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.

  Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.
   
 3. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana Mzizi Mkavu, nadhan utakuwa umetusaidia wengi sana.
   
Loading...