Ramlis
JF-Expert Member
- Aug 22, 2013
- 597
- 496
Kipindi cha nyuma nilikuwa natumia pirate bay blowser app kushusha mafaili ya torrent katika simu yangu ikaja ikagoma, ikawa inaandika "proxie unavailable" nikaweka kickass pro ikawa inafanya kazi vuzuri na zote hizo app zilikuwa na speed kubwa hadi mb 2 kwa sek, kwa sasa hii app nayo haifanyi kazi nimejaribu kila njia hata kui-update bado haifanyi kazi, nimebadili hadi simu lakni bado vilevile hadi nimeamua kutumia app zingine za kushusha file za torrent lakni hizi zinasumbua sana. Kuna sehemu niliwahi kusoma kuwa ukitaka Kudownload torrent file kwa uharaka angalia "seeders" zikiwa nyingi na speed inaongezeka na zikiwa kidogo vilele speed inapungua. Kwa upande wangu hilo sijalifatilia hadi sasa, kinachonisibu ni pale ninapotaka kushusha kitu kutoka torrent unakuta file husika lina zaidi ya mwaka speed yake haizidi kb 50 nimejaribu kubadili aina tofauti ya app za torrent lakni hakuna madiliko na kama lina miaka mingi hata kuhesabu byte 1 haiwezekani. Kama file ni la chini ya mwaka mmoja sana sana ndani ya miezi 3 speed yake huwa kubwa sana. Kwa mfano movie ya 2009 ni ngumu kuikuta ina miezi sita hadi mwaka tangu imepandishwa mtandaoni.
Naombeni msaada wenu juu ya hili kama linaweza kurekebishwa au njia yoyote ya kushusha torrent file lolote kwa speed kwa kutumia simu.
NB:
Kwa sasa ni siku ya tatu ninashusha season ya 49 days ya mwaka 2011 ina gb 3.6 na hadi sasa ina gb 1.8 iliyoshushwa tu na mtandao hapa nilipo huwa speed inafikia mb 6 kwa sek, na leo hii nimepakua windows 10 ina gb 3.72 ndani ya dk 23 ilikuwa imekamilika.