Msaada juu ya ununuzi wa bati za msouth..!

iconman

Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
28
Reaction score
13
Wana Jamii forum nimefanikiwa kujenga nyumba yangu sasa niko ktk hatua ya kuezeka nilikuwa nataka nitumie bati zile za rangi alimaarufu kama bati za msouth nilikuwa naomba ushauri wenu je kampun/kiwanda gani hapa bongo kinatoa bati nzuri za aina hiyo na kwa bei nzuri na je ntagunduaje bati feki na original na mwisho rangi gani huwa inavutia sana ukitumia kuezeka.
 
Rangi nzuri ni deep blue,
Tumia bati za Alaf za IT (Msouth) gauge 28,ni imara,ngumu na hazipauki,kama unahitaji ni pm nikupe namba ya agent wa Alaf anayeuza bati hizo kama uko dar.
 
Hakuna haja ya Agent, kwa aina hii ya bati (IT) ni vema akaenda moja kwa moja ALAF pale karibu na Tazara kama yupo DSM.
 
Lakini mkuu nijuavyo hizo bati almaarufu msouth original ni pale tu NABAKI AFRICA karibia na kiwanda cha Coca Cola Dar ila wana matawi hata mikoani. Wengine wanaiga tu! Hayo ya alaf ni mabati ya kawaida......ni rangi tu.
 
NABAKI AFRICA Wanauza bati zinazofanana muundo na vigae,
ALAF wanauza za migongo mipana kwa maana ya IT.
 
Rangi nzuri ni deep blue,
Tumia bati za Alaf za IT (Msouth) gauge 28,ni imara,ngumu na hazipauki,kama unahitaji ni pm nikupe namba ya agent wa Alaf anayeuza bati hizo kama uko dar.

Ahsante mkuu ngoja ntajaribu kuwacheki hao ALAF
 
18,500 kwa kipande kimoja..nyumba ya kawaida ni vipande 400 mpaka 600 piga hesabu mkuu
 
Nunua za ALAF ndo nzuri..pia kama utahitaji fundi mzuri wa kuezeka ni pm...kaniezekea yangu vizuri sana
 
Wana Jamii forum nimefanikiwa kujenga nyumba yangu sasa niko ktk hatua ya kuezeka nilikuwa nataka nitumie bati zile za rangi alimaarufu kama bati za msouth nilikuwa naomba ushauri wenu je kampun/kiwanda gani hapa bongo kinatoa bati nzuri za aina hiyo na kwa bei nzuri na je ntagunduaje bati feki na original na mwisho rangi gani huwa inavutia sana ukitumia kuezeka.
Yaan we unauliza rangi gani nzuri..??! si uangalie 3D computer model yake inasemaje..??! au haukuwa na michoro wewe..??!, na kwanza kama ni hivyo umepataje Building permit..??! unafanya mammbo kienyeji sio..??! we una kesi ya kujibu kwa jamhuri...!!!
 
Lakini mkuu nijuavyo hizo bati almaarufu msouth original ni pale tu NABAKI AFRICA karibia na kiwanda cha Coca Cola Dar ila wana matawi hata mikoani. Wengine wanaiga tu! Hayo ya alaf ni mabati ya kawaida......ni rangi tu.

hivyo ni vitu viwili tofauti!!
 
Wekeni bei za NABAKI NA ALAF ndo ombi la jamaa yetu

Nilinunua mwezi uliopita (July) bati za ALAF aina ya IT.
  • Bei ya mita moja gauge 28 ni Tsh 13,800/- VAT inclusive
  • Order: maximum ni siku 7, lakini nilizipata ndani ya siku tatu tu. Unatoa order pale ofisini na kulipia halafu wakisha iandaa wanakupigia simu kwenda kuchukua.
  • usikupende kupitia madalali, nenda moja kwa moja ofisini kwao.

Cha muhimu ni kumaliza kazi ya kenchi, fundi anapima urefu na idadi ya mabati halafu unaenda ALAF.

All the best.
 
Nunua za ALAF ndo nzuri..pia kama utahitaji fundi mzuri wa kuezeka ni pm...kaniezekea yangu vizuri sana

Sawa mkuu ngoja ni jaribu kuwacheki hao nasikia wanauza kwa meta je hao jamaa wa ALAF wanauza meta 1 bei gan au wanafanyaje mauzo yao..!
 
Nilinunua mwezi uliopita (July) bati za ALAF aina ya IT.
  • Bei ya mita moja gauge 28 ni Tsh 13,800/- VAT inclusive
  • Order: maximum ni siku 7, lakini nilizipata ndani ya siku tatu tu. Unatoa order pale ofisini na kulipia halafu wakisha iandaa wanakupigia simu kwenda kuchukua.
  • usikupende kupitia madalali, nenda moja kwa moja ofisini kwao.

Cha muhimu ni kumaliza kazi ya kenchi, fundi anapima urefu na idadi ya mabati halafu unaenda ALAF.

All the best.

Ahsante mkuu bagain hawa jamaa wa ALAF hizo ofisi zao ziko maeneo gan hapa mjini
 
Ofisi za ALAF zipo nyuma ya soko la Vetenary, soko hili liko upande wa kushoto wa barabara ya Mandera ukiwa unatokea buguruni na baada ya kuvuka junction ya Tazara.
 
Back
Top Bottom