Msaada juu ya kilimo cha tumbaku Chunya, mtaji na nianze na shamba la ukubwa gani?

PeterLugomo

Member
Aug 27, 2015
19
17
Habari wakulima, mimi naomba kupata mawazo chanya juu ya kilimo cha tumbaku hasa kwa mkoa wa mbeya wilayani chunya maana nimeelekezwa huko kilimo kinakubali.

Kwa wazoefu na hili zao naomba uzoefu wenu.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Chunya walikuwa wanalima tumbaku ya moshi na kwa sasa wanalima tumbaku ya mvuke, kuhusu mbegu makampuni yanayonunua hua yanagawa katika vyama vya msingi miezi miwili kabla ya msimu wa mvua, nadhani kuhusu pembejeo na elimu huwa inatolewa, pembejeo hukopeshwa katika vyama vya msingi kama ndio mdhamini baada ya mrajisi wa mkoa kujiridhisha makadirio ya uzalishaji. Karibu
 
Asante sana kaka nimepata mwanzo. Masoko ni kuuzia makampuni tu au na serikali inanuua.
 
Chunya walikuwa wanalima tumbaku ya moshi na kwa sasa wanalima tumbaku ya mvuke, kuhusu mbegu makampuni yanayonunua hua yanagawa katika vyama vya msingi miezi miwili kabla ya msimu wa mvua, nadhani kuhusu pembejeo na elimu huwa inatolewa, pembejeo hukopeshwa katika vyama vya msingi kama ndio mdhamini baada ya mrajisi wa mkoa kujiridhisha makadirio ya uzalishaji. Karibu
Maelezo mazuri.Nimewahi kufanya Kazi huko km Afisa Kilimo.Ulichosema ni sahihi,labda km utaratibu umebadilika sasa hivi.
 
Unatakiwa uwe kwenye ushirika
Ukiwa kwenye ushirika unapewa kila kitu unakopeshwa.

Utakacho kuwa nacho wewe ni Shamba na mabani ya kuchomea tu
 
Na ushirikina au kumwomba Mungu, kati ya hayo.

Nakujua vizuri tu Kule...Lupa,matwiga,upendo,biti manyanga n.k
 
Back
Top Bottom