Msaada jinsi ya kuunganisha wireless mouse na USB receiver ya mouse tofauti

Msaada jinsi ya kuunganisha wireless mouse na USB receiver ya mouse tofauti

kateka

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2012
Posts
697
Reaction score
549
Kama mada inavyojieleza hapo juu, ni kwamba nina wireless mouse ambayo nilipoteza usb receiver, sasa nimepata USB receiver ya mouse tofauti nimejaribu kadri ya uwezo wangu kuunganisha sijafanikiwa, nawaita wataalamu wote wa mambo ya IT mnisaidie hii kitu ili niweze kuendelea na matumizi ya kawaida. Msaada wenu unahitajika tafadhari.
 
Yaan unachojaribu kufanya ni kama kuweka petroli kwenye gari la diesel ukitegemea litembee
 
Yaan hum utajibiwa majibu mpaka ukimbie, wewe nunua mpya no altenative, zipo mpaka za elf20
 
Haziingiliani hata za brand moja mara nyingi haziingiliani, fikiria kama mko watu wawili chumba kimoja mnatumia brand hiyo hiyo zingeingiliana ingekuwa shida. Logitech wana baadhi ya mouse zina technolojia wanaita Unifying unaweza kutumia adapter moja device tofauti.
Kama hiyo mouse ni bluetooth unaweza kutumia na bluetooth yoyote ila wireless mouse nyingi sio bluetooth.
 
Umeiweka Vizuri sana Mkuu, nimekupata, kumbe hii Unifying ni kwa kampuni ya Logitech tu!!!!!
 
siku nyengine nunua za bluetooth hasa 4.0 kupanda. itakaa na chaji hadi miezi 6, pia bluetooth una pair tu na adapter ya ndani, na speed yake inakuwa nzuri compare na hizi cheap wifi mouse.
Ahsante Mkuu, vipi hizi za bluetooth ni brand gani mkuu?
 
Back
Top Bottom